|
Kundi la
mawakili, wanaharakati na wanasayansi nchini Brazil limewasilisha ombi mahakama
ya juu nchini humo likitaka wanawake wenye virusi vya Zika waruhusiwe kutoa
mimba.
|
Virusi
vya Zika vinaaminika kusababisha watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo, na
kudumaza ubongo.
Utoaji
mimba nchini Brazil hauruhusiwi kisheria, ila tu wakati wa dharura ya kiafya au
iwapo mimba imetokana na ubakaji hali ambayo kwa Kiingereza inajulikana kama
microcephaly.
Hata
hivyo mwaka 2012, uliruhusiwa kwa watu walioathiriwa na ugonjwa mwingine wa
ubongo kwa jina anencephaly.
Wataalamu
wameonya kwamba idadi ya watu walioambukizwa na virusi vya Zika mwaka huu
huenda ikafikia kati ya milioni tatu au nne katika mabara ya Amerika.
Ombi
hilo mpya litawasilishwa mahakama ya juu katika kipindi cha miezi miwili.
Kundi
linaloandaa ombi hilo ndilo lililowasilisha ombi kwa niaba ya waathiriwa wa
anencephaly mwaka 2012 mahakama ya juu na kupata ushindi.
Wakati hayo yakijiri, Thomas Bach, mkuu wa
Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki amesema hatua zinachukuliwa kulinda michezo ya
mwaka huu ambayo itaandaliwa mjini Rio de Janeiro.
IOC itatoa mwongozo kwa wanariadha na
wageni ambao wanapanga kushiriki au kuhudhuria michezo hiyo, Brazil ndilo taifa
lililoathirika zaidi na mlipuko wa Zika ambapo inaelezwa kuwa kwa mujibu wa
wizara ya afya nchini humo zaidi ya watoto 200 wamezaliwa wakiwa na vichwa vidogo
ambavyo vimethibitishwa, huku wengine
zaidi ya 3,000 wakiendelea kuchunguzwa.
Watu wengi
walio athiriwa na virusi hivyo huwa hawaonyeshi dalili za kuambukizwa virusi
vya Zika lakini wanaweza kusambaza virusi hivyo kwa watoto walioko tumboni.
Hadi sasa bado hakuna tiba wala chanjo
dhidi ya ugonjwa huo hivo Marekani imesema inatumai itaanza kufanyia majaribio
chanjo katika mwili wa binadamu kufikia mwisho wa 2016.
|
Muonekano wa mtoto mwenye ugonjwa wa Zika |
Dalili za Zika
Homa
Vipele
Maumivu kwenye maungio
Macho kuwa mekundu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni