Alhamisi, 21 Januari 2016

Makatibu watuhumiwa kuwaibia fedha wakulima - Rungwe


Mkulima wa zao la chai wilayani Rungwe


Wakulima wadogo wadogo   wa zao  la chai (RSTGA)  katika   sikimu  ya Mwakaleli  wilayani  Rungwe   Mkoani  Mbeya  wameshauriwa  kujiunga na  benki  za  wakulima   ambazo  zimeanzishwa  katika  maeneo tofauti  wilayani  humo   kwa   lengo  la  kuondokana na  utapeli  wa fedha  zao.

Hayo  yamesemwa  na  baadhi  ya    viongozi  wa  benki  za  wakulima wadogo wa zao hilo  wilayani  humo  wakati  wakitoa  elimu kwa  wakulima  juu  ya  kujiunga  na benki  hizo ambazo  zitawasaidia katika    kujikwamua  na  hali  ya kiuchumi   ikiwa  ni pamoja na kuondokana na migogoro  isiyo  ya lazima.

Hamisi mwakibete ambae ni meneja  wa   benki  ya   lwangwa  na   kandete ,alisema   kila  mkulima  anapaswa   kuchukua  hatua   ya  kujiunga   na benki  hizo  ili  kuondoa  matatizo ambayo  yamekuwa   yakijitokeza wakati wa  kugawana  fedha  kutoka  kwa  makatibu wao.

‘’kumekuwa  na migogoro mingi  ambayo  imekuwa  ikijitokeza  baina  ya wakulima  na   makatibu pindi  wanapokuwa  wakigawana  fedha, kwani  Makatibu  waliowengi wamekuwa   wakificha  pesa   za  wakulima kutokana  na kwamba   baadhi ya   wakulima  hawana  uwezo  mzuri wa  kufanya  mahesabu na  hiyo ndio  sababu  kubwa  ya  wao
kutapeliwa  fedha  zao bila  wao kujua’’ alisema  mwakibete.

Alisema     licha    ya  wakulima   kukatwa  pesa  zao  lakini   bado kumekuwa na  adha  ya makatibu kutekwa pindi wanaporejea kutoka benk kuchukua fedha zilizotunzwa na wakulima   hali inayo hatarisha usalama wa makatibu pia kudhoofisha uchumi wa wakulima

Esau Mwangomora  mmoja wa wakulima  wa zao  hilo   wilayani humo, alisema  makatibu  wamekuwa  wakiwafyeka  fedha  zao kutokana  na uelewa wao kuwa mdogo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni