Alhamisi, 21 Januari 2016

Shindano la tuzo ya ubobezi wa fikra za afrika (The Master Mind) kutambulishwa rasmi Tarehe 26/1/2016


Taasisi ya Dream Success Enterprises  (Njozi ya Mafanikio) yenye makao yake makuu jijini Dar es salaam inatarajia kutambulisha shindano jipya la tuzo ya ubobezi wa fikra za afrika (The African Master Mind)  mapema tarehe 26/1/2016 ambapo utambulisho huo utafanyika mbele ya waandishi katika ukumbi wa Idara ya habari maelezo uliopo jijini dar es salam na kuanza rasmi siku hiyo,

Hayo yamesemwa na dr. Joshua Lawrence ambae ni mkurugenzi wa mipango na mikakati wa taasisi hiyo alipokua akizungumza na Blog hii,

Dr. Lawrence amesema tuzo hiyo itatolewa kwa watu ambao watakua wameonyesha mawazo chanya ya namna ya kuisaidia Afrika iweze kupiga hatua za maendeleo,
Akielezea kuhusu vigezo vya kushiriki katika  tuzo hii dr,  Lawrence alisema  mtu yeyote  awe ni mwanamke au wanaume wenye umri kuanzia miaka kumi na sita (16) na kuendelea anaruhusiwa kushiriki bila kujali kiwango cha elimu na kwamba kinacho angaliwa ni fikra.

Akifafanua zaidi kuhusu namna unavyoweza kushiriki alisema mshiriki atatakiwa kuji rekodi sauti na picha (video clip) isiyozidi  dakika kumi (10) akielezea kwanini afrika pamoja na kua na rasilimali za kila namna bado watu wake wangali masikini na tutafanyaje ili tutoke hapa? ambapo washiriki wata ruhusiwa kutumia lugha ya Kifaransa, Kiingereza au Kiswahili, Kisha ataituma clip hiyo katika whatsApp namba 0744- 683-511,

Aidha amesema kua zaidi ya milioni mia tano (500ml) zitatolewa kwa wale ambao watashiriki ambapo washindi watakabidhiwa tuzo ya kombe ambalo litakua ni ukumbusho wa ushiriki wake huku wale watakao fikia  kumi bora clip zao zitaingizwa kwenye video katika mfumo wa dokumentari (documentary) kisha zitasambazwa katika nchi za afrika,

Dr. Joshua alimaliza kwa kuelezea uzoefu wa taasisi hiyo katika kuandaa tuzo mbali mbali nchini ambapo alitaja baadhi ya tuzo ambazo zimewahi tolewa na taasisi ya Dream success enterprises (njozi ya mafanikio) kua ni pamoja na tuzo ya SHUJAA KATI YETU ambapo mtunukiwa wa kwanza wa tuzo hiyo alikua ni mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali bw. Ludovick Utouh ambae kwa sasa amestaafu,

tuzo nyingine ya SHUJAA KATI YETU ilitolewa mwaka jana 2015 kwa watu watatu  na miongoni mwa washindi wa tuzo hiyo ni Vicky Mtetema aliekua mtangazaji wa BBC ambae alipewa tuzo kutokana na ubunifu na ujasiri wake wa kupambana na kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi(albino)  wanapewa haki yao na kulindwa,

Saed Kubenea ambae alipewa tuzo ya umahili wa kuandika habari na kutumia kalamu katika kuelimisha umma na mtu mwingine aliye pewa tuzo hiyo Mh. David Kafulila ambae alipewa tuzo kutokana na ujarisi wake katika suala zima la kuhakikisha kwamba watanzania wananufaika na rasilimali zilizomo hasa katika scandle ya ESCROW

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni