Jumatano, 27 Januari 2016

SERIKALI NCHINI ERITREA YASEMA MWANAMKE ATAKAE MZUIA MUMEWE KUOA MKE MWINGINE ATAKABILIA NA ADHABU YA KIFUNGO CHA MAISHA








Serikali ya Eritrea imetunga sheria inayowalazimisha wanaume wote nchini humo kuoa wanawake kuanzia wawili na kuendelea na kwamba watakaokaidi agizo hilo watakabiliwa na kifungo cha maisha jela. 

Katika taarifa rasmi ya serikali, serikali hiyo imewataka wanaume kuhakikisha inafuata sheria hiyo na serikali imeahidi kugharamia sherehe zote za harusi pamoja na nyumba kwa wanandoa wapya. 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya serikali, sheria hiyo imetungwa kutokana kuwepo kwa uhaba wa wanaume nchini humo unaotokana na vita kati ya nchi hiyo na Ethiopia. 

“Mwanamke ambaye atajaribu kumzuia mme wake kuoa mwanamke mwigine ataadhibiwa kwa kupewa kifungo cha maisha jela,” inasomeka sehemu ya nyaraka hiyo ya serikali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni