Ukojozi
kitandani unaweza kusababisha matatizo ya kitabia kwa sababu mtoto anaweza
kuhisi ana makosa na kujisikia aibu. Ni kweli kwamba mwanao anatakiwa
kuwajibika kwa kitendo hicho cha kukojoa kitandani (hii ina maana mwanao
anatakiwa kufanya usafi). Lakini usimfanye mwanao ahisi kwamba yeye ndio mwenye
makosa.Ni muhimu kwa mwanao kujua kwamba ukojozi kitandani siyo kosa lake.
Kitendo cha kumuadhibu mwanao kwa kosa la kukojoa kitandani haitasaidia kutatua
tatizo.
Itamsaidia
mwanao kujua kwamba hakuna anayejua sababu kubwa inayopelekea ukojozi
kitandani.Muelimishe kwamba mambo hayo hutokea katika familia (Kwa mfano, kama
mwanao akikojoa kitandani, unatakiwa kujadiliana naye na kumhaidi kumsaidia
kupambana na hali hiyo).
Msisitizie
mwanao kwamba anatakiwa aende msalani wakati wa usiku. Muwekee taa kuelekea
msalani ili imuwie rahisi kuona njia ya kuelekea msalani. Unaweza pia
kumfunika na blanketi pamoja na tandiko lingine la plastiki ili iwe rahisi
zaidi wakati wa kufanya usafi.Endapo mwanao atajaribu kukusaidia, msifie kwa
kujaribu na kwa kusaidia kufanya usafi.
Hata hivyo, utafiti wa hivi karibuni Desemba 2014 uliofanywa na shirika
la habari la Reuters, unaonyesha kuwa kuwapa adhabu kali au kuwapiga watoto
vikojozi mara kwa mara kwa kunaweza kuwa sababishia magonjwa sugu kama vile
saratani, pumu na magonjwa ya moyo.
UKOJOZI KITANDANI KWA
WATOTO
(Bed-Wetting)
-Enuresis
Nini
maana ya Enuresisi?
Enuresisi
ni neno la kitaalamu linalomaanisha hali ya kutoa mkojo bila ridhaa ya
muhusika(involuntary),aina mojawapo tuliyoizoea ni ukojozi kitandani wakati mtu
akiwa amelala hasa wakati wa usiku.
Ukojozi
kitandani huwapata zaidi watoto na mara nyingi ni hali ya kawaida tu katika
ukuaji wao. Ukojozi kitandani hutokea zaidi kwa watoto wa kiume kuliko wa kike.
Vitu
gani husababisha ukojozi kitandani?
Kuna
sababu nyingi zinazoweza kusababisha ukojozi kitandani. Baadhi ya njia hizo ni
hizi zifuatazo:
·
Kurithi (Katika familia)
·
Kushindwa kuamka kutoka usingizini
·
Msongo wa mawazo
·
Ukuaji wa taratibu wa mishipa za fahamu kutofanya kazi inavyotakiwa
·
( hali ambayo humpunguzia mtoto uwezo wa kuzuia kibofu kutoa mkojo)
·
Matatizo ya homoni (kuzalishwa katika kiwango kidogo kwa homoni
zinazopunguza kuzalishwa kwa mkojo wakati wa usiku)
·
Maambukizi katika njia ya mkojo
·
Matatizo katika mrija wa mkojo kwa wavulana au kwenye njia ya mkojo kwa
wavulana na wasichana.
·
Matatizo kwenye uti wa mgongo
·
Kibofu cha mkojo kuwa kidogo
Ukojozi
kitandani sio tatizo la akili au tabia. Tatizo hili halitokei eti kwa sababu
mtoto ni mvivu kiasi kwamba hawezi kuamka kitandani na kwenda msalani.
Je
ni kipindi gani watoto wengi huweza kudhibiti hali ya mahitaji ya kukojoa?
Watoto huweza kudhibiti kibofu cha mkojo katika umri tofauti. Wakifikia umri wa miaka 6, watoto wengi huacha kukojoa kitandani. Ukojozi wa kitandani hadi katika umri wa miaka 6 siyo kitendo cha ajabu, ingawa inaweza kuwanyima amani wazazi na walezi wengi.Kama mtoto yuko chini ya umri wa miaka 6, tiba kwa tatizo la ukojozi kitandani kwa kawaida siyo mara nyingi watoto wengi huacha kukojoa bila aina yoyote ya matibabu.
Watoto huweza kudhibiti kibofu cha mkojo katika umri tofauti. Wakifikia umri wa miaka 6, watoto wengi huacha kukojoa kitandani. Ukojozi wa kitandani hadi katika umri wa miaka 6 siyo kitendo cha ajabu, ingawa inaweza kuwanyima amani wazazi na walezi wengi.Kama mtoto yuko chini ya umri wa miaka 6, tiba kwa tatizo la ukojozi kitandani kwa kawaida siyo mara nyingi watoto wengi huacha kukojoa bila aina yoyote ya matibabu.
Daktari anaweza
kusaidia lolote?
Ingawa
watoto wengi wanaokojoa kitandani hawana tatizo lolote la kiafya, daktari
anaweza kusaidia kugundua kama tatizo la mtoto wako kukojoa kitandani
linasababishwa na matatizo mbalimbali ya kiafya. Kwanza daktari atakuuliza
iwapo mwanao hukojoa mchana na usiku. Halafu daktari atampima na anaweza
kuchukua vipimo vya mkojo kuangalia kama kuna maambukizi au kisukari au
matatizo mengine.
Daktari
anaweza kutaka kujua mwenendo wa kimaisha wa mwanao anapokuwa nyumbani na hata
shuleni.Ingawa unaweza kuogopa mtoto wako anapokojoa kitandani, tafiti
zimeonyesha kuwa sio rahisi kwa watoto wanaokojoa kitandani kuwa na matatizo ya
hisia tofauti na watoto wengine wasio kojoa kitandani.Daktari pia atakuuliza
jinsi mnavyoishi katika familia kwa sababu m matibabu yanaweza kuhusisha
mabadiliko kadhaa ya kimaisha hapo nyumbani.
Je
kuna matibabu yoyote kwa tatizo la ukojozi kitandani?
Watoto
wengi huacha kukojoa kitandani bila kupata matibabu yoyote.Ingawa wakati
mwingine wewe na daktari wako anayemuona mtoto wako mnaweza kuamua kwamba mtoto
anahitaji tiba fulani.Kuna aina 2 za tiba: kumbadili mtoto kitabia, na kumpatia
dawa.
Kumbadili
mwanao kitabia husaidia kumfanya mwanao aache tabia ya kukojoa kitandani.
Baadhi ya njia za
kumbadili mwanao kitabia ni hizi zifuatazo:
·
Mzuie mwanao asinywe vinywaji/maji kwa wingi kabla ya kulala
·
Hakikisha mwanao anenda msalani kila mara kabla ya muda wa kulala na pia
mara tu anapo anza kusinzia.
·
Tumia kengele itakayolia pindi kitanda kinapolowa ,hii humfundisha mtoto
kufahamu pindi kibofu kinapojaa wakati wa usiku
·
Mpe zawadi mtoto anapoamka bila kukojoa kitandani
·
Mwambie mtoto wako kubadili matandiko mwenyewe kila anapokojoa kitandani
·
Mpe mwanao mazoezi ya kibofu: muelekeze mwanao akae muda mrefu bila
kukojoa kipidi cha mchana, ili kibofu kiwe na uwezo wa kutunza mkojo mwingi
zaidi
Ni dawa gani
zinazotumika kutibu ukojozi kitandani?
Daktari
wako anaweza kumpa mwanao dawa kama ana umri wa miaka zaidi ya saba(7)
iwapo njia za kumbadilisha kitabia zilizotajwa hapo hazijasaidia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni