rubani Rogers Gower enzi za uhai wake |
Helikopta (chopa) iliyotunguliwa |
Mahakama
ya Wilaya ya Bariadi imewahukumu watu wanne, mmoja kifungo cha miaka 20 jela na
watatu miaka 15 kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya hatia ya kukutwa na
silaha ambazo zilitumika kutungua helikopta kwenye Pori la Akiba Maswa wilayani
Meatu na kusababisha kifo cha rubani wake Rogers Gower raia wa Uingereza,
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi
wa Wilaya ya Simiyu Mary Mrio alisema anawapa adhabu hiyo washtakiwa hao baada
ya kukiri kosa la kukutwa na silaha hiyo kinyume cha sheria na hivyo
kutoisumbua mahakama.
Katika hukumu hiyo, Njile Gunga
ambaye anadaiwa kutungua ndege hiyo Januari 29 atatumikia kifungo cha miaka 20,
huku akisubiri kesi nyingine mbili ya mauaji ya rubani na uhujumu uchumi ambazo zitatajwa Mahakama ya
Mkoa wa Simiyu.
Waliohukumiwa
kifungo hicho mbele ya Hakimu Mkazi wa wilaya, Mary Mliyo, ni Mange Buluma
(47), Shija Mjika (38), Dotto Pangali (41) na Njile Gunga (28), ambao
wamehukumiwa kutumika kifungo cha miaka 15 jela kila mmoja kwa kosa la pili
kati ya makosa 11 waliyoshtakiwa.
Hakimu
Mliyo alisema kesi hiyo iliyokuwa na washtakiwa tisa, wengine walikana makosa
yao yakiwamo ya kukutwa na silaha na risasi ambao ni, Mange Buluma, Moses
Masasi na Mwigulu Kanga, hivyo kurudishwa mahabusu na kesi yao itaendelea
Februari 24, mwaka huu.
Wakili Mwandamizi wa Serikali,
Yamiko Mlekano alitaja makosa hayo kuwa ni kumiliki na kukutwa na silaha
kinyume cha sheria.
Shtaka la tatu ni kukamatwa na
risasi tano za bunduki aina ya rifle, shtaka ambalo Pangali na Gunga walikiri.
Katika shtaka la nne linalowakabili
washtakiwa wote wanne, Wakili Mlekano alidai ni umiliki risasi kinyume cha
sheria, ambazo walikamatwa nazo Februari 8 na bunduki aina ya Rifle 303.
Washtakiwa hao waliomba kupunguziwa
adhabu kwa kile walidai ni mara yao ya kwanza kutenda makosa kama hayo, lakini
Mlekano aliomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine.
Hakimu Mrio alisema kwa kosa la
kwanza, pili na nne mahakama inawahukumu kifungo cha miaka mitano jela kila
mmoja, kosa la tatu miaka mitano au kulipa faini ya Sh10 milioni.
Ikumbukwe
kuwa washtakiwa hao walifikishwa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi kwa mara ya
kwanza Februari 10, mwaka huu kwa kosa la kutungua helikopta 'chopa' na
kusababisha kifo cha rubani wake, katika pori la akiba la Maswa wilayani Meatu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni