Jumapili, 21 Februari 2016

Wapinzani wampa wakati mgumu rais Piter Mtharika wa Malawi, wampa siku 90, awe amefungasha virago vyake Ikulu,

Na Ephraim Banda:

Dr. Joyce Banda - kiongozi wa chama cha People's Party (PP) 

Dr. Lazarus Chakwera - Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Malawi na Rais wa chama cha Malawi Congress Party (MCP)


Bw. Griffin Botha - Mwenyekiti wa vijana wa Malawi waishio Tanzania 

Vyama vya upinzani nchini Malawi Malawi
 Congress Party na People's party kinachoongozwa na Joyce Banda vimempa siku 90 rais wa inchi hiyo kuachia madaraka kwa madai kua rais Piter Mtharika ameshindwa kuongoza taifa hilo.


Kwamujibu watarifa ya pamoja iliyo tolewa na vyama hivo haijaweka bayana kwamba watafanya nini endapo rais huo hato ng'atuka madarakani.

Afisa habari wa ikulu ya Malawi Bwana Gerald Viola amenukuliwa na vyombo vya habari nchini Malawi akisema rais Mtharika alichaguliwa na wananchi wa Malawi sio vyama, na kuongeza kwamba vyama hivyo vinataka kupotosha wana inchi,

Chama cha upinzani cha United Democratic Front UDF kinachoongozwa na rais msitafu Bakali Muluzi ambacho kwa sasa kinaongozwa na mwanaye Atupele Muluzi ambaye ni mwanasheria pia wao wameungana na serekali ya Mtharika na wanafanya kazi pamoja.

Bw. Griffin Botha ambaye ni Mwenyekiti wa vijana waki Malawi waishiwo nchini Tanzania amesema vyama hivo havina mamlaka ya kumuondoa rais madarakani, pia alisema ni wananchi peke wenyewe mamlaka ya kumuondoa rais madarakani.

Botha alisema kwamba kwasababu inchi ya Malawi ina utawala wa ki Demokirasiya hivo kila mtu anaweza kutoa mawazo yake katika utawala kisiasa ambapo aliwataka wananchi wa Malawi kua na utulivu na kutosikiliza mameno ya vyama vinavyotaka kupotosha wananchi

Ikumbukwe kwamba kipindi cha utawala wa marehemu Bingu Wamtharika siku kama hizo 90 zilisha wahi tolewa kwa rais huyo na kipindi hicho lilitolewa na Public Afairs Committee PAC lakini tamko hilo halikuza matunda,

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni