Madiwani
wa Halmashauri ya Mbeya vijijini wamegoma kupitisha kifungu cha bajeti ya
kumnunulia mwanasheria wa halmashauri suti ya Tsh. 500,000 kila mwezi.
Awali
akiwakilisha
bajeti ya
mwaka 2016/2017 kwenye Baraza la Madiwani kwa niaba ya Mkurugenzi wa
halmashauri Mbeya Vijijini, Mwanasheria Prosper Msivala alisema kila mkuu wa
idara atapata Tsh. 180,000 kwa ajili ya mawasiliano huku wanasheria wakipewa
sh. 500,000.
Msivala
alisema suti ya mwanasheria ni pamoja na viatu, shati, suruali na koti pamoja
na skafu yake
Diwani
wa Maendeleo Mbeya Vijijini, Daniel Mwanyamale alipinga mwanasheria kushonewa
sare kila mwezi kwa sh500,000
Aliwataka
waandaaji wa bajeti hiyo kuangalia upya suala hilo na kwamba hata suala la
kupewa sh. 180,000 za mawasialiano litazamwe upya kwani halikubaliki
Diwani
Ramadhi Jelambaa alisema afadhali feza hizo zipelekwe kwenye shughuli za
maendeleo ukiwamo ujenzi wa madarasa na ununuzi wa dawa za vituo na zahanati
Hata
hivyo Mwanasheria Msivala alitetea fedha hizo akisema ni jukumu la halmashauri
kutoa na kuwaomba madiwani wapitishe bajeti hiyo
“Ndugu
zangu kila mwanasheria anapoajiriwa katika halmashauri yetu ni lazima kila
mwanasheria apate sh500,000 na hilo lipo kisheria,” alisema Msivala
Ikumbukwe wakati hilo liki jiri la baraza la madiwani kupinga kupitisha kifungu cha bajeti ya mwanasheria kununuliwa suti inayoghalimu kiasi cha sh,500,00 kila mwezi huku madiwani wakipewa kiasi cha sh.180,000 kwa mwezi kwa ajili ya mawasiliano.
Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amekua akisisitiza matumizi mazuri ya fedha za umma huku akiwa wajibisha haraka iwezekanavyo baadhi ya viongozi wanaothibitika kutumia vibaya fedha za umma,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni