Jumanne, 22 Machi 2016

Baada ya matokeo ya Meya wa jiji la Dar kutangazwa Freeman Mbowe azungumzia kauli ya Rais "Acha demokrasia ichukue nafasi"

Meya wa Jiji Isaya Mwita Charles 
Meya wa Jiji Isaya Mwita Charles anayeungwa mkono na Ukawa ndiye Meya wa Jiji la Dar baada ya kupata kura 84 dhidi ya Yenga Omari (CCM) aliyepata kura 67.

Akizungumza na waandishi mara baada ya kutangazwa mshindi Mwita amesema kua nchi yetu itapiga hatua kubwa haswa jiji la Dar Es Salaam  endapo viongozi na wananchi watashirikiana na  kuweka pembeni itikati za vyama.

Mwita amesema kua kwa kua Rais John Pombe Magufuli ametabainisha kua anataka kuwasaidia watanzania hivo kwa kushirikiana kwa pamoja na kuweka itikati pembeni nchi itapiga hatua.   

Nae Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Freeman Mbowe akizungumza mara baada ya matokeo kutangazwa na Chadema kuibuka na ushindi amesema ushindi wao haujatokana na kauli la Rais ambayo aliitoa jana Ikulu

Rais magufuli alisema acha demodrasia ichukue nafasi yake” akimaanisha kua demokrasia itumike kumpata Meya Jiji hilo, kauli hiyo imeibua hisia kua huenda imechangia kuipa ushindi Chadema

Mbowe amesema kua ushindi wao umetokana na kura za wananchi kwani  Rais amekuwepo kwa kipindi miezi mitano huku akishuhudia ufedhuli ambao umekua ukitendeka katika mchakato wa kumpata Meya,
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Freeman Mbowe 

Chadema kimepata ushindi katika uchaguzi wa umeya wa Dar es salaam baada ya uchaguzi huo kuahirishwa kwa mara kadhaa. Hii ni mara ya kwanza kwa CCM kushindwa kutwaa kiti cha meya.

Aidha mara baada ya matokeo kutangazwa kuliibuka nderemo na vifijo kutoka wananchi kufurahia ushindi huo wa Bw. Mwita 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni