Hiki ndio chumba kilichokua na miili yote mitatu ya marehemu hao |
haya ndio maelezo yao waliyo yaandika katika daftari la wageni katika gesti waliyo kua wamefikia |
Polisi wakitoa miili ya marehemu (siku ya jumapili) |
Gari lililobeba miili ya marehemu hao kutoka hospitali ya Kyela kuipeleka Mbeya mjini |
Kaka wa marehemu Zauda Omari na Baraka Chaula ambao ni ndugu (kaka na dada |
Mwenye kikoi cha kimaasai ndie mume wa marehemu Zauda Omar |
Kaka wa marehemu Zauda Omari na Baraka Chaula ambao ni ndugu (kaka na dada akiwa katika majonzi makubwa |
Maiti
za watu watatu waliouawa kikatili baada ya kunyongwa na miili yao kuchomwa moto
ndani ya chumba kimoja zimetambuliwa, wamo ndugu wa familia moja.
Wakati
taarifa ya jeshi la polisi iliyotolewa juzi na Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya,
Ahmed Msangi, ikiwataja marehemu hao kuwa ni Mariam Hassan, Abbas yasini na
Tatizo Adamu wote wakazi wa Songea, Mkoani Ruvuma.
Hata
hivyo, baada ya ndugu hao wa marehemu kuwatambua, wametaja majina halisi ya
marehemu hao na kusema kuwa si wakazi wa Songea, bali wote ni wakazi wa Jijini
Mbeya katika maeneo ya Ilomba na Mbarali, na kwamba si wafanyabiashara kama
walivyokua wamejiandikisha wao katika daftari la wageni katika gesti waliokua
wamefikia.
Akizungumza
kwa niaba ya familia, Riziki Chaula, aliyejitambulisha kuwa ni kaka wa marehemu
wawili, aliwataja marehemu hao kuwa ni Zauda Omar (34) , Mkazi wa Ilomba,
Jijini Mbeya na Baraka Chaula (28) Mkazi wa kijiji cha Utulo kata ya Mapogolo,
Wilayani Mbarali ambao ni ndugu.
Alimtaja
marehemu watatu kuwa ni Rodgers Simwaka, Mkazi wa Ilomba, Jijini Mbeya na
kwamba ni jirani wa marehemu Zauda na amekuwa akijihusisha na shughuli za
kusajili laini za simu katika maeneo mbalimbali Mkoani Mbeya.
Aliongeza
kuwa, mbali na marehemu Zauda kuwa ni mdogo wake waliochangia baba, lakini pia
alikuwa ni mke wa mtu na hadi mauti inamfika walikuwa wakiishi kwa amani na mumewe
aliyemtaja kwa jina la Abdalah Malifyuma.
“Vifo
hivi vimetuacha kwenye mkanganyiko mkubwa sana….kwani Zauda na Baraka ni dada
na kaka mtu na huyo mwingine ni jirani yao, sasa iweje watoke Mbeya hadi Kyela
na kukutwa wakiwa wamenyongwa ndani ya chumba kimoja” alihoji Riziki.
Aidha,
Riziki aliongeza kuwa, siku moja kabla ya tukio marehemu Zaudi alikuwa
amewasiliana na majirani zake, pamoja na mumewe na kuwaaga kuwa alikuwa na
safari ya kwenda na kurudi Wilayani Rungwe.
Licha
ya majirani wa marehemu Zauda kusimulia jinsi walivomfahamu marehemu na kuishi
naye, lakini mume wa marehemu huyo alikataa kuzungumza chochote juu ya tukio
hilo la mauaji, huku muda wote akionekana kulia kwa hisia kali.
Mmoja
wa majirani wa marehemu Zauda, Said Nkenja alisema siku moja kabla ya tukio
marehemu alimtaarifu kuwa angesafiri
kwenda kwenye shughuli zake Mjini Tukuyu, Wilayani Rungwe na kwamba taarifa za
kuuawa kwake zimewashitua na kuzua hofu kubwa.
Kwa
upande wake, rafiki wa karibu na marehemu Rodgers, aliyejitambulisha kwa jina
la Sebastian Aman, alisema siku mbili kabla ya tukio la kuuawa kikatili kwa
rafiki yake ambaye walikuwa wakifanya kazi ya kuuza laini za simu, alimuaga
kuwa atakua na safari kikazi ya siku
tatu ya kwenda Wilayani Chunya.
Mganga
Mfawidhi wa hospitali ya Wilaya ya Kyela, Dk.Frencis Mhagama, alithibitisha
miili ya marehemu hao kutambuliwa na kuchukuliwa na ndugu zao baada ya kukaa
hospitalini hapo kwa siku 3
Maiti
hizo zilikutwa kwenye chumba kimoja zikiwa zimefungwa mifuko ya rambo usoni huku
zikiwaka moto.
Hata
hivyo bado chanzo cha mauaji hayo ya kikatili hakija julikana haswa ukizingatia wawili ni ndugu mmoja kati yao ni jirani, swali je? walikua na agenda gani huko kyela ukizingatia alikuwepo kaka na dada akiwemo jirani, kwanini wote walidanganya kuhusu eneo wanalotarajia kwenda pindi walipo waaga majirani kabla ya safari? ni nani alietekeleza unyama huo je ndie aliewaita huko?.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni