kisaikolojia inaelezwa kuwa, wakati mwingine hisia ni adui kwa
sababu huweza kukudumbukiza kwenye anasa na hatimaye kujikuta unakwama kwenye
kutimiza malengo yako. Hebu tuangalie 4 kihisia ambazo zimewafanya wengi
washindwe kufikia malengo yao.
Ulishawahi kukaa na kujiuliza ni jinsi gani hisia
zako zinaweza kukusukuma ukafanya jambo ambalo hukulitegemea? Huenda
hujajiuliza lakini nikwambie tu kuwa hisia ni adui mkubwa wa maendeleo ya
binadamu hasa kama utashindwa kuzizuia zisiathiri maisha yako.
HISIA 4 ZINAZOWEZA MALENGO YAKO
Furaha
iliyopitiliza
Hali hii inapokutokea hujiona ni mtu unayeweza kufanya lolote lakini pia
unaweza kujikuta unashindwa kufikia malengo mazuri uliyojipangia.
Mfano: Unadhani ni kwa nini kwenye mabaa na kasino wanatumia
muziki mkubwa na kunakuwa na kelele nyingi? Hii yote ni ili kukufanya upate
hisia ya furaha inayoweza kukusukuma kutumia mshahara wote hapo baa.
Hii ni kwa sababu kwa wakati huo una furaha kupitiliza kutokana na mazingira
hayo, unajikuta unasahau malengo yako na hata shida za nyumbani.
mtu anapoenda sehemu za starehe katika vivyaji anaanza kwa kujinunulia yeye na watu
alioongozana nao, furaha ikizidi anaanza kugawa pombe kila meza akiamini ana hela nyingi kumbe zile pesa ni
kwa ajili ya matumizi yaliyomfanya achukue mkopo.
Wasiwasi
Hii ni hisia nyingine mbaya ambayo inaweza kukusababishia ukaharibu mali zako
na hata maisha kwa ujumla.
Wasiwasi katika maisha ya binadamu wakati mwingine husaidia lakini wakati
mwingine huharibu mambo kabisa.
Unaweza kuwa unataka kufanya mabadiliko labda ya ofisi yako kwa kutumia fedha
nyingi lakini usifanye lolote tu pale hali ya wasiwasi itakapokuingia kwani
unahisi huenda ukiitumia fedha haitarudi. Huyu ni adui mkubwa na hakika huwezi
kufikia malengo yako kama utakuwa ni mtu mwenye wasiwasi kila wakati.
Utakuta mtu anataka kufungua duka lakini anashindwa kwa kuhofia kuwa atakosa
wateja na hela alizoziandaa kufungulia duka zikaenda bure, ‘huyu wasiwasi’ bado
atakuwa ni adui kwa sababu haukupi nafasi ya kufanya jambo .
Huzuni
ukiwa na huzuni mara nyingi uwezo wa kufikiria na kupanga malengo huwa ni mdogo
sana.
Hivi hujawahi kuona ukiwa na huzuni unatamani kulala tu au kwenda baa kukutana
na watu, ingawa wengine huwa hawapendi hata kukutana na watu?
Hasira na kuhisi kuonewa
Hisia hizi ni hatari zaidi ya zote kwani kama usipokuwa mwangalifu unaweza
kujikuta unafanya jambo ambalo si zuri kabisa, ukajihatarishia maisha yako na
hata ya familia yako kwa ujumla.
Unaambiwa ukiwa na hasira usimtumie ujumbe wa sms mtu aliye kuudhi au usiongee
mbele za watu maana unaweza kujikuta unadharaulika kwa maneno utakayo yatoa.
Ndiyo maana unashauriwa kutuliza hisia zako kwanza kabla ya kufanya jambo
lolote linaloyahusu maisha. Kamwe usiruhusu hisia zikatawala maisha yako.
Kibinadamu huwezi kuishi bila kupatwa na hisia hizo lakini kikubwa cha kufanya
ni kuhakikisha unazituliza ili zisije zikakuletea madhara,
Ukihisi una furaha
nyingi kaa mbali na pesa zako, ukiwa na huzuni jaribu kuwa karibu na watu wanaoweza
kuipoteza kama siyo kuipunguza hali hiyo, ukiwa na wasiwasi pia washirikishe
watu waliowahi kupitia mambo hayo watakushauri pia, lakini ukiwa na hasira
fanya kila uwezalo kuzipunguza ikiwa ni pamoja na kunywa maji mengi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni