Ijumaa, 18 Machi 2016

Kwa atakae watambua ndugu, jamaa wa mama huyu anaombwa atoe ushirikiano wa hali na mali

akiwa katika soko la Melini Handeni - Tanga, mara nyingi huenda kuomba msaada wa chakula hapo
Eneo la makaburini ambalo amekua akilitumia mama huyo  kupika na kuhifadhi vyombo anavyo tumia 
Eneo la makaburini ambalo amekua akilitumia mama huyo  kupika na kuhifadhi vyombo anavyo tumia

Mama anaeonekana katika picha hizo amekua akijitambulisha kwa jina la mama Pili yupo Handeni mkoani Tanga amekua akiishi na kulala nje ya Hospital ya wilaya ya Handeni kwa muda mrefu.

Pia amejitengea sehemu ya kupikia nje kidogo ya makaburi yaliyopo mkabala na Hospitali hiyo, kwa haraka haraka ukimuona anaonekana kama mtu mwenye tatizo la mtindio wa ubongo lakini amekua akikabiliwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu kisha zinamjia.

Inaelezwa kua kwa watu waliomuona wakati akiwasili katika eneo hilo wanadai alikuwa mzima lakini kadri siku zilivyokua zikienda ndivyo alivyokua akibadilika na kuonekana kama mtu anaekabiliwa na msongo wa mawazo au mtindio wa akili, pia anaonekana kama mtu aliepotea katika mazingira ya kutatanisha 

wenyeji wa eneo hilo wanasema katika mazungumzo yake mama huyo anawakumbuka na kuwataja mara kwa mara watu hawa ambao kwa mujibu wa maelezo yake ni wanawe 1. Pili, 2. Mwanne, 3. Jumanne.

Lakini pia anataja sana jina la Mwanawande na wande pamoja na kutamka mke mwenza mara kwa mara katika maongezi bila kumtaja jina huyo mke mwenzie ni nani

Mwanamke huyu amekua akijaribu kujieleza kua anatokea Nzega bila kufafanua ni Nzega ipi jambo ambalo limekua ni gumu kubaini kama ni Nzega ya Iringa au Tabora.

Atakayemtambua mama huyu au kuwajua ndugu zake tafadhari wasiliana kwa no.0715 55 94 33 au 0675 602877 na 0656766796.

Muandishi wa Blog hii alipata taarifa za mama huyu kupitia jukwaa la waandishi wa habari wanawake ambalo limekua likiendeshwa kwa njia ya mtandao wa kijamii WhatsApp (women journalist)

Baada ya taarifa  kuhusu mama huyo waandishi walijadili ili kuweza kubaini iwapo taarifa ya uwepo wa mama huyo ina ukweli au laa hivo baada ya kujadili hilo aliombwa muandishi wa habari alieko jijini Tanga aweze kufuatilia ili kupata ukweli

Lakini kutokana na umbali wa eneo la tukio muandishi huyo alilazimika kumuagiza mtu ili aweze kufuatilia habari hiyo ambapo alithibitisha kua mama huyo yupo kama iliyo elezwa,

Muwakilishi huyo alizungumza na baadhi ya  wakazi wa eneo hilo la Handeni Tanga ambapo walikiri kutambua uwepo wa mama huyo,

Wakielezea namna ambavyo wamekua wakimchukulia mama, uwepo wake na mazingira anayo ishi hapo Handeni Tanga wakazi hao walisema kua wanamchukulia kama mtu wa usalama wa taarifa

“nimeulizia bado yupo na kwakuwa ni Handeni na mimi nipo Tanga mjini hivo nimemtuma mtu akazungumze nae leo ili tuelewe kama ni msongo wa mawazo au la ili tujiridhishe, kwani wenyeji wa hapo Handeni wanamchukulia kwamba ni mtu wa usalama wa taifa hivo hapo yuko kazini. Kwa hiyo nitawajuza zaidi” huu ni ujumbe na muandishi baada ya kufuatilia suala hilo

Naomba tushikiriane ili ndugu zake waweze kupata taarifa hii na kumsaidia, sambaza taarifa hii kwa kadri uwezavyo! 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni