Kamishna wa
Jeshi la Plisi Zanzibar Hamdan Omar Makame akizungumza na waandishi wa Habari
kuhusu ulipuaji wa mabomu ulio tokea leo
|
Waandishi wa habari wakimsikiliza Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar |
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame akizungumza na
waandishi wa Habari kuhusu matokeo ya uripuaji wa mabomu na kuchoma moto nyumba
na maskani za CCM Unguja na Pemba.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kamishna wa Jeshi la
Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame leo Zanzibar.
Nyumba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame
imeripuliwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu na watu
wasiojulikana majira ya saa 5.00 usiku huko Kijichi nje kidogo ya mji wa
Zanzibar.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Ofisini kwake Makao Makuu ya
Polisi Kilimani, Kamishna Hamdani amesema tukio hilo limeathiri sehemu ya paa
la nyumba na dari na kujeruhi baadhi ya watu waliokuwa
wamelala na kusababisha hasara kubwa.
Amesema tukio hilo linafanana lile lililotokea tarehe 03 mwezi huu katika
Maskani ya CCM Kisonge Unguja hivyo polisi inaendelea kufanya uchunguzi ikiwa
ni pamoja na kuwasaka wahalifu wanaofanya uhalifu huo.
Akizungumzia matukio mengine ya uhalifu na kuchoma moto
nyumba, maskani na kituo cha Afya huko Pemba, alisema Jeshi la Polisi
limeanza msako mkali na kuwatia mbaroni watu 31 ambao wanaendelea kuhojiwa na
watakaohusika watafikishwa katika vyombo vya sheria.
Kamishna Hamdani amewatowa hofu wananchi kuhusu usalama wao na mali
zao kuelekea uchaguzi wa marudio utakaofanyika tarehe 20 mwezi huu na kuwepo
kwa ongezeko la askari katika maeneo mengi ya mijini na vijijini ni
moja ya juhudi za kuimarisha ulinzi na kuhakikisha
uchaguzi huo utakuwa salama na amani.
Ametahadharisha kuwa mtu yoyote atakayejihusisha kuanziasha vurugu au
kufanya kitendo chenye ishara ya uvunjifu wa amani atapambambana na
vyombo vya sheria.
Kamishna
Hamdani ametoa wito kwa wananchi waliojiandikisha kupiga kura kujitokeza kwa
wingi siku hiyo ili waweze kutimiza haki yao ya msingi ya kikatiba bila ya
woga kwani jeshi hilo limejipanga kuimarisha ulinzi katika idala zote
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni