Waziri wa Katiba na sheria Malawi Samuel Batson Tembenu
Kufuatia
taarifa mbali mbali za kumshutumu rais wa Malawi Mutharika kukwepa kujibu maswali
kutoka kwa wabunge katika bunge linalo endelea nchini humo na ku chapishwa
katika magazeti kwa vichwa vya “Mutharika Akwepa maswali ya wabunge “na “
Mutharika akana kujibu maswali ya wabunge”.
Maneno hayo yamekuja baada ya Speaker wa bunge la Malawi Richard
Msowoya kutangaza kwamba rais Mutharika amewapa majumu mawaziri wake kujibu
maswali bungeni kwa niamba yake, wabunge wengine waliomba muongozo wakisheria
na katiba kwa kusema kwamba sheria iko wazi kabisa kwamba kuna mambo mengine
ambayo raisi hawezi ku wakilishwa.
Hata kama sheria hiyo inasema hivyo haimuzuwiyi rais kuwakilishwa popote pale,
kulingana na maswali ya wabunge hao waziri wa sheria na katiba wa Malawi Samuel Batson
Tembenu alisema rais haja vunja sheria yoyote ile isipokua ambacho
amekifanya ni kutekeleza wajibu wake kwa kugawa majukumu yake kwa mawaziri wa serikali
yake.
Tembenu
pia alisema “sio lazima rais aje bungeni kujibu maswali yakutoka kwenu wabunge
rais anakazi nyingi ambazo anatakiwa kuzifanya ofisini kwakwe kitendo
alichokifanya rais ku wapa mawaziri nguvu za kumuwakilisha yeye bungeni na sio
kosa kisheria rais” alisema Waziri Tembenu.
Sheria
za bunge la Malawi zina ruhusu rais kwenda bungeni na kujibu maswali kutoka kwa
wabunge jambo ambalo wabunge wengine wanasema Mutharika amekiuka sheria, muhadhili
moja kutoka chuo kikuu cha Malawi amesema, inawezekana Mutharika ameogopa kubanwa
na maswali kutoka kwa wabunge wa upinzani, hususani kuhusu swala la njaa linalo
kumba inchi hiyo.
Wengine
wanasema huenda Mutharika anatumia Taluma yake ya uwamasheria kutokana na kwamba
anajua sheria vizuri na kwamba kwa sababu yeye ni mkufunzi wa sheria.
Hata kama sheria hiyo ipo haijawahi kutokea rais wa nchi hiyo kwenda bungeni kujibu
maswali bungeni, endapo Mutharika angekubari kwenda bungeni na kuulizwa maswali
angekua rais wa kwanza kujibu maswali ya papo kwa hapo.
Tembenu
alimalizia kusema kwamba kazi ya mawaziri ni kumuwakilisha rais, na kwamba
mawaziri wanafanya kazi na rais na rais anawa amini ndio maana wamepewa kazi ya
kum wakilisha.
Endapo
rais Mutharika alitakiwa kwenda bungeni kujibu maswali papo kwa hapo jumatano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni