Alhamisi, 31 Machi 2016

Kiti kalia Rais Magufuli katika mgahawa Mwanza chawa dili, Meneje wa Mgahawa huo aelezea jinsi alivyopata oda ya chakula kwa ajili ya msafara wa Rais.



Mgahwa alioutumia Rais John Magufuli kupata mlo wa mchana na msafara wake  kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza, umekuwa kivutio kwa wateja wengi wakinunua chakula na kutaka kukalia kiti na meza aliyotumia kiongozi huyo

meneja wa mghahawa huo wa victoria, Elizabeth Maneno alisema kwamba hali hiyo ilijitokeza mara baada ya rais kuondoka hapo.

"hata leo tumepokea wateja wengi kulinganisha na siku nyingine, baadhi yao wanaagiza chakula kwa sharti la kutaka kukikalia kiti na meza aliyotumia Rais Magufuli" alisema Elizabeth.

akizungumzia hali ilivyokuwa juzi kabla na wakati wa ugeni huo meneja huyo alisema, "ilikua ni hofu na woga uliochanganyika na furaha kumwona Rais akiingia kwenye mghahawa wetu wa chai ya rangi ya Sh200 na ya maziwa sh300.

"Mshtuko wetu uligeuka furaha baada ya kubaini kuwa oda ya sahani 28 za kubeba (takeaway),tulizoagizwa mapema asubuhi bila kuelezwa zinakoenda zilikuwa za ujumbe wa Rais," aliongeza kuwa

"kabla ya Rais magufuli hajaingia kwenye mgahawa wetu alikuja mtu mmoja tusiyemfahamu na kuagiza sahani 28 za chakuala kwa gharama ya sh 5,000 kila mmoja,"

alisema baada ya kumtaarifu mteja wake kuwa chakula kiko tayari, alielekezwa kuandaa meza na viti kwa sababu wageni wake (wateja), sasa wameamua kula palepale mgahawani.

"Ghafla tulimwona Rais aanaingia ndani ya mghahawa wetu, kwanza tulishikwa na hofu, woga na kihoro tusijue tunafanyaje nini hadi tulipogutushwa na aliyetoa oda kwa kutuagiza tugawe chakula alichoagiza," alisema meneja huyo. "hapo ndipo tulipobaini kumbe chakula kile kilikua cha ugeni wa Rais."

aliye muhudumia Rais

"Ingawa nimewahi kumhudumia (Rais) akiwa mbunge na waziri, hii ilikuwa kwa mara yangu ya kwanza na pengine inaweza kuwa ya mwisho ingawa siombei iwe hivyo kumhudumia akiwa Rais," alisema Hamida Miraji aliyemuhudumia Dk Magufuli na mkewe Mama Janeth.

Pamoja na chai ya rangi na ya maziwa mghahawa huo pia unauza vyakula vya aina mbali mbali kwa bei kati ya sh.1,500 hadi sh5,000 kwa vyakula vya kubeba, huku soda ikiuzwa kwa sh500 kwa chupa.

Kubadili jina la mgahawa
"Bado hatujaamua ingawa tangu juzi watu hawapaiti tena Victoria, bali mghahawa wa Magufuli, labda mkurugenzi anaweza kuamua hili," alisema Elizabeth.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni