KWA NINI VIJANA WA MJINI HAWAFANIKIWI?.
Inawezekana na wewe umekuwa ukijiuliza swali
hili lililokuwa likinitatiza kila siku kwamba kwa nini vijana wengi wanaoishi
mjini huwa hawafanikiwi kama wale wanaotoka vijijini na kuja mjini?
Hili ni jambo linalowatesa watu wengi,
wengine wamekuwa wakilalamika kwamba kwa nini fulani ametoka kijijini, kaja
mjini kafanikiwa na wakati wao ni maborn town lakini bado wamepigika kitaa.
Nimefanya uchunguzi, nimezungumza na vijana
wengi na nimefanikiwa kupata baadhi ya majibu ambayo leo hii ningependa
kuzungumza nawe, labda tushauriane mawili-matatu, kama kuna hatua za kuchukua,
basi uchukue ili na wewe ufike pale unapotakiwa kufika.
Kumbuka kwamba mimi pia nilizaliwa kijijini,
nikakulia huko, nikaondoka na kuja Dar es Salaam ambapo sikuwa na ndugu, mvua
zilikuwa zangu na jua lilikuwa langu. Sikuwa na pa kwenda, katika kituo cha
mabasi ya mkoani (KISUTU) hapo zamani ndipo nilipokuwa nikilala. Niliumwa sana
na mbu, lakini katika hayo yote, sikujuta, maumivu niliyosikia nilijipa moyo
kwamba kuna siku yangekoma, kweli,
leo unapozungumza watu waliyoyabadilisha
maisha yao kutoka kijijini na kuja mjini, basi mtoto wa mkulima, mimi pia
nitakuwepo kwenye orodha hiyo. Hebu ngoja nikwambie kwa nini vijana wengi wa
mjini hawafanikiwi kirahisi.
Hizi ndio
sababu
KUJISHTUKIA Mjini kuna ajira nyingi kuliko
vijijini ambapo ajira yao ni moja tu, kulima. Vijana wengi waliozaliwa mjini
huwa hawafanikiwi kirahisi kwa kuwa wanajishtukia. Leo unaweza ukamwambia
kijana wa mjini auze sabuni kwa kutembeza, lakini anaogopa, anamuonea aibu mtu
fulani atamuona, lakini biashara hiyohiyo, mtu kutoka kijijini anafanikiwa na
mwisho wa siku anaachwa kijana wa mjini akilalamika.
Unapoamua kutafuta maisha, usiogope kuchekwa,
usiogope kudharaulika. Najua wengi hawataki kubezwa wanapofanya biashara za
kutembeza pipi au nyingine, lakini kumbukeni kwamba hata matajiri wakubwa
mnaowaona katika Tanzania hii, wameanzia hukohuko, kwenye biashara ndogo,
zikakua na kuanzisha kubwa. STAREHE Hii nayo ni sababu mojawapo.
Vijana wengi wa mjini, baada ya kupata fedha
kidogo, wanachokifikiria ni starehe tu. Kijana wa mjini yupo radhi atumie hata
elfu hamsini kwa usiku mmoja tu na wakati kiasi anachoingiza ni kidogo. Kabla
ya kufanya matumizi makubwa, hebu jiulize, je kuna umuhimu wa kufanya hivyo?
Kama unataka kwenda sehemu kula bata kwa hamsini hiyo, hebu jiulize, je
usipokwenda siku hiyo, utakufa? Je usipotumia kiasi hicho cha fedha maisha yatakwisha?
Je utachekwa? Kama jibu lako ni hapa, basi achana nalo, acha fedha zako ziwe
akiba na zikusaidie hapo baadaye.
Unapoanza starehe, kunywa pombe kupindukia,
huwezi kufanikiwa, kila siku utakuwa mtu wa kulalamika. Nafurahi kumuona kijana
akiendesha gari, lakini wakati anaendesha gari, nafurahi zaidi kumuona akiwa na
biashara inayomuingizia kipato kikubwa. Huwa sifurahii kumuona kijana
akiendesha gari, huku mafuta akitumia mshahara wake. Mtu kama huyu kufanikiwa
ni vigumu, acha mshahara ufanye mambo mengine, gari ni gharama, wakati mwingine
linaharibika, linahitaji vifaa vya gharama, je mshahara ndiyo utakaotumika tu?
Na kama ndiyo, je fedha za matumizi na kufanyia mambo mengine zitatoka wapi?
KUJISAHAU Ndiyo! Wengine wanajisahau. Kama
leo mtu akafanya kitu kikamuingizia laki moja, basi kesho hawezi kufanya kitu
kama hicho, atakwambia mpaka fedha hizo ziishe kwanza. Hivi umekwishajiuliza
kwa nini makonda wengi wa daladala hawafanikiwi? Wengi wanapata fedha nyingi,
kwa siku konda anaweza kupata hata shilingi elfu thelathini mpaka hamsini,
kweli mtu wa namna hiyo hawezi kufanikiwa? Kuna mtu anafanya kazi kwa mshahara
wa laki mbili, na anafanikiwa, kwa nini mtu kama konda hafanikiwi? Nimewahi
kukutana na makonda wengi, kauli zao ni kwamba wanapata fedha kila siku, leo
akipata elfu hamsini, kesho inaingia nyingine sasa kwa nini niiweke hii ya leo?
Ukisikiliza sababu zao unaweza kuona zina mashiko lakini hazina mashiko yoyote.
Mchukulie mtu kama Mengi au matajiri wengine,
wanaingiza kiasi gani? Mbona wanajua kuweka akiba na huwasikii wakisema leo
imeingia hii, nitumie yote kwa kuwa kesho itaingia nyingine?
Ni lazima fedha tunazozipata tuziweke
matumizi sahihi na tusijisahau kwa kujipa moyo kwamba kesho itaingia nyingine.
Kama tukipambana, tukiingiza fedha na kufanyia vitu vya msingi, tusiporidhika,
tusipojisahau basi hii Tanzania itakuwa na mabilionea wengi sana na kila kijana
atakuwa na maisha mazuri.
KUKOSA UBUNIFU Kuna wengine wanapata fedha
lakini wanapofungua biashara, wanakosa ubunifu. Kabla ya kufungua biashara
fulani ni lazima uangalie je ukiifungua biashara hiyo sehemu fulani, utapata
wateja? Je biashara hiyo inahitajika mahali hapo? Huwezi kufungua baa sehemu
yenye vijiwe vya wahuni, watu wataogopa kuja kwa kuwa wanaogopa kukabwa! Huwezi
kufungua duka sehemu isiyokuwa na nyumba zaidi ya kumi, unapoamua kufungua
biashara, ni lazima uangalie sehemu na kisha ufanye ubunifu. Hapo ndipo ambapo
vijana wengi wamekuwa wakifeli, wengine wana
UBUNIFU Kuna wengine wanapata fedha lakini
wanapofungua biashara, wanakosa ubunifu. Kabla ya kufungua biashara fulani ni
lazima uangalie je ukiifungua biashara hiyo sehemu fulani, utapata wateja? Je
biashara hiyo inahitajika mahali hapo? Huwezi kufungua baa sehemu yenye vijiwe
vya wahuni, watu wataogopa kuja kwa kuwa wanaogopa kukabwa! Huwezi kufungua
duka sehemu isiyokuwa na nyumba zaidi ya kumi, unapoamua kufungua biashara, ni
lazima uangalie sehemu na kisha ufanye ubunifu. Hapo ndipo ambapo vijana wengi
wamekuwa wakifeli, wengine wanaamua kuanzisha biashara ya mandazi sehemu ambayo
kuna wauzaji wengi wa mandazi, je unapotaka kuanzisha biashara hiyo sehemu kama
hiyo, unaweza kufanya ubunifu? Kama unaweza, fanya ila kama hauwezi, achana
nayo.
Jirani anauza mandazi, na wewe hapa
unaanzisha biashara ya mandazi, unahisi utaweza kupata wateja? Ni lazima ufanye
ubunifu, yaani kama mtu anauza mandazi, angalia udhaifu wake, kama mandazi yake
ni ya kawaida, yako yaweke hiriki, yako yafanye yawe makubwa, huo ndiyo
ubunifu. Kama unataka kuanzisha biashara ya chipsi, angalia udhaifu wa
mwenzako. Yeye anauza chipsi bila mishikaki, wewe weka na mishikaki, kama
anauza chipsi bila samaki, wewe weka na samaki.
Siyo yeye hana samaki, na wewe
huna, yeye hata soseji, na wewe huna, yeye hana mishikaki, na wewe huna, ni
lazima ufanye ubunifu. Sasa vijana wengi wa mjini wamekosa vitu hivyo na mbaya
zaidi wengi wao hawataki kushaurika. Hili linawakosti sana na ndiyo maana wengi
huanzisha biashara na kuanguka chini. Kwa leo acha niishie hapa, natumaini
vijana wa mjini mtafanyia kazi yale machache niliyoshauri.
Asanteni. SHIGONGO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni