Na
jana ndio wakanirejesha kule kule waliponichukua karibu na kituo cha Taxi cha
airport wakiwa wamenifunika uso na kunitupa tu saa 11.30 Alfajiri nilipojifunua
ndio nikajikuta nipo hapo nikajiburura hadi kituoni nikaongea na mama mmoja
hapo anisaidia akanambia kaa chini mwangu akawa ananiliwaza ndio baadae
nikachukua taxi kwenda Aga khan hospitali daktari wangu hakuwepo ikabidi niende
Regence Hospitali tokea asubuhi hadi hiyo saa 10 alipokuja Onesmo kunichukua na
kwenda polisi kuweka taarifa na kuhojiwa hadi saa 4 usiku. Simu yangu muda
mwingi nilikuwa nayo mwenyewe na ndio siku ya mwanzo nilipoongea walipokuja
wakanipiga sana sana na muda mwingine simu wakaizima ila hawakuichukua na
hawajachukua chochote kwa kuwa walisema shida yao nisiripoti uchaguzi tu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni