habari
na Ephraim Mkali.
Joyce Banda |
Ken Msonda |
Khumbo Kachali |
Kiwewe
na uchu wa madaraka umeingia ndani ya Chama tawala cha zamani nchini Malawi cha
People (PP),
chama
hicho kinasemekana kusimamisha kazi aliyekua kua Katibu Mkuu wa chama hicho
Bwana Ken Msonda kwa madai kua anashirikiana na alieye kua makamu wa rais
katika utawara wa Joyce Banda bw. Khumbo Kachali, kuleta mpasuko ndani ya chama
hicho.
Msonda
amefanya kazi ya ukatibu Mkuu wa chama hicho kwa miaka miwili, kwa sasa chama
hicho kimemteua Joseph Chikwamba kua katibu tawara mpya,
Uteuzi
huo umethibitishwa kwa vyombo vya habari na katibu Mkuu wa chama hicho Bwana
Ibrahim Matola na kusema ''ni jambo la kawaida chama kufanya mabadiliko''
Akizungumza
na muandishi wa habari hii Msonda amesema kwamba kwamba yeye haja ng'olewa na
uongozi wa chama bali alijiudhulu mweyewe kwenye kiti hicho cha ukatibu mkuu
tawara
''Nashanga
kwamba chama kinasema kwamba kimenisimanisha kazi wakati mimi nimeomba
kupumzika tena kwa barua, leo hii wanatangaza kwamba wamenisimamisha, nashanga
kabisa'' alisema Msonda.
Pia
Msonda alikanusha taarifa za kwamba yeye amekua anafanya mikutano ya siri na
Kachali ya kupanga mbinu za kumuondoa Joyce Banda kwenye chama hicho.
Miezi
kadha iliyopita wajumbe wengine wa mkutano mkuu wa chama hicho walinukuliwa
wakisema Joyce Banda anatakiwa kurudi nyumbani Malawi ambapo kwa sasa yuko mafichoni
tangu alipo anguka katika uchaguzi uliofanyika Mei 2014.
Tangu
Joyce Banda aondoke kwenda mafichoni mambo mengi yamekua yaki jitokeza ndani ya
chama chake hicho ambapo aliyekua mugombea mwenza katika uchaguzi wa mwaka 2014
Sositen Gwengwe alikihama chama hicho na ku jiunga na chama cha Malawi
Congress,
Hadi
sasa haijulikani lini Joyce Banda atarejea nyumbani kujenga na kuimarisha chama
chake.
Mhadhiri
wa maswala ya siasa katika chuo kikuu cha Chancellor College Professor Bone
Dulani amesema kuna umuhimu Joyce Banda kurudi nyumbani kujenga chama chake lakini
pia amemtaka Banda kumteua kiongozi moja atakae simamia chama hicho hadi pale atakaporejea nyumbani.
Kwa
tarifa zilizo patikana kuhusu Joyce Banda zisema anashindwa kurejea Malawi
kutoka alikojificha kwa kuhofia kufunguliwa mashitaka ya ubadhilifu wa fedha
uliotokea katika utawara wake.
Hivi
karibuni vyombo vya habari nchini Malawi vilimnukuu mume wa rais mstafu Joyce
Banda Jaji Mkuu mstafu Richard Banda akisema usalama wa mke wake ni mdogo
endapo mke wake atarudi Malawi.
Katiba
ya nchi ya Malawi haijaweka kinga kwa rais kuto shitakiwa baada ya kuachia
madaraka, rais wa kwanza kushitakiwa nchini Malawi alikua Bakili Muluzi na mali
zake zingine zili taifishwa kutokana na kuhujumu uchumi kulikojitokeza katika
kipindi chake cha utawala mwaka 1994 hadi 2003
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni