JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, TAASISI YA KUZUIA NA
KUPAMBANA NA RUSHWA
TAARIFA
KWA UMMA WABUNGE WATATU WAJUMBE WA KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA
WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI KWA RUSHWA
Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imewafikisha Mahakamani wabunge
watatu ambao ni wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa kwa kosa la
kushawishi na kuomba rushwa ya Shilingi Milioni thelathini (30,000,000/-) kinyume
na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007 kifungu cha 15
(i)(a).
Wabunge
hao ni Mheshimiwa Suleiman Ahmed Saddiq Mbunge wa Mvomero ; Mheshimiwa Victor
Mwambalaswa Mbunge wa Lupa na Mheshimiwa Kangi Lugola Mbunge wa Mwibara.
Wabunge
hao wamesomewa shitaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu
Mfawidhi, Mh.Thomas Simba.
Akisoma
mashtaka hayo wakili wa TAKUKURU, Maghera Ndimbo akishirikiana na Emmanuel
Jacob alisema kuwa mnamo Machi 3, 2016 majira ya saa 2 - 4 usiku, katika Hotel
ya Golden Tulip iliyopo jijini Dar es Salaam washtakiwa wote watatu waliomba
rushwa ya shilingi Mil.30 kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo kwa
lengo la kumsaidia ili Taarifa ya Halmashauri hiyo ambayo ilikuwa kwa wakati
huo ijadiliwe tahere 16/3/2016 ipitishwe bila marekebisho.
Uchunguzi
wa shauri hili bado unaendelea na washtakiwa wote watatu mahakama imewaachia
kwa dhamana ya kila mtuhumiwa kuwa na mdhamini mmoja na kulipa shilingi milioni
5. Kesi imeahirishwa hadi tarehe 14/4/ 2016 itakapotajwa tena.
TAKUKURU
inawajulisha wananchi wote kwamba hakuna mtu ambaye yupo juu ya Sheria. Rushwa
haivumiliki!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni