Na Asha Athuman, Mbozi
|
Mkuu wa mkoa wa Songwe bi. Chiku Gallawa akisaini kitabu cha wageni |
Mkuu wa Mkoa Mstaafu Abbas Kandoro akimkabidhi kalablasha Mkuu wa Mkoa Songwe Bi. Chiku Gallawa |
Kiongozi wa Machifu Wilaya ya Mbozi, Chifu Nzunda akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Songwe Bi. Chiku Gallawa |
Baadhi ya viongozi walio hudhuria katika tukio hilo la Makabidhiano ya Mkoa Mpya wa Songwe |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mstaafu ndugu
Abbas Kandoro amekemea tabia ya wananchi
kutumia fujo, na vitendo vinavyo
hatarisha amani katika kudai haki au kushinikiza jambo fulani lifanyike.
Akizungumza katika makabidhiano
ya mkoa Mpya wa Songwe yaliyofanyika jana tar 1.4.2016 katika Wilaya ya Mbozi, Kandoro
amewataka wananchi kujenga utaratibu wa kuzuia jazba na kufanya fujo katika kudai haki na badala watumie hekima ili kulinda amani na utulivu, kwakua amani na utulivu ni
muhimili wa kupiga hatua katika maendeleo.
Kandoro amesema historia inaonesha
jamii yeyote ambayo imekua ikijihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani daima haina
maendeleo.
Hata hivvo amewataka viongozi
wa dini, mila na serikali kushirikiana kwa pamoja kutoa elimu kwa jamii ili
kutokomeza imani za kishirikina, ulevi,wivu na ujambazi.
Kandoro amesema Takwimu
zinaonyesha kua Wilaya ya Mbozi imekua ikijihusisha na mauaji ya kikatili huku chanzo chake kikiwa ni imani za
kishirikina,
Hata hivyo amewaaga na kuwashukuru
wananchi wa Mkoa mpya wa Songwe kwa ushirikiano mkubwa walio mpa kwa kipindi
chote ambacho amekua akiwatumikia wananchi wa Mkoa wa Mbeya na Mkoa mpya wa
Songwe kabla ya kugawanywa na kua Mikoa miwili.
amesema hakuna marefu yasiyo na
ncha kwa mtumishi yeyote yule haswa
ambae amechaguliwa ameteuliwa au kuajiriwa hivyo ni lazima atambue kua kuna
ukomo katika uwajibikaji wake.
Kandoro amewashukuru watanzania
na serikali kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kuwatumikia kwa kipindi cha miaka
arobaini (40) ambapo amemshukuru mwenyezi mungu kwa kua amestaafu akiwa bado ana
nguvu na afya njema ambayo inamuwezesha kuendelea kuwajibika baada ya kustaafu.
Ametoa wito kwa watumishi wote nchini kuzitumia vema nyazfa
zao ili pindi ukifika ukomo wao wa kuwatumika wananchi waondoke kwa amani.
Kandoro amesema baada ya
kustaafu atakwenda kuendeleza kauli mbiu ya Mh. Rais John Pombe Magufuli “HAPA KAZI TU” kwa kua amestaafu kuwa tumikia wananchi lakini kimsingi bado anahitaji kuwajibika kwa
ajili ya maisha yake kwani tumbo daima litaendelea kudai kupata chochote.
Hata hivo Kandoro amempongeza Bi.
Chiku Gallawa, kwa kuteuliwa kuwa Mkuu
wa Mkoa Mpya wa Songwe lakini pia kwa kua muanzilishi wa mkoa huo ambao una
wilaya nne (4), halmashauri tano (5), Tarafa kumi na mbili (12), kata sabini na
nne (74), vijiji mia tatu na saba (307) na mitaa sabini na moja (71) ambapo
alimkabidhi kalablasha lenye maelezo na changamoto zinazo ukabili Mkoa huo mpya
wa Songwe.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Songwe Bi. Chiku Gallawa amesema anatambua kua hakuna sehemu isiyokua na
changamoto na kwamba changamoto ndizo zinatusukuma katika maendeleo haswa
zainapogeuzwa kua fursa.
Akizungumzia baadhi ya
changamoto ambazo zilibainishwa kama ukosefu wa miundo mbinu, imani za
kishirikina, vitendo vya uvunjifu wa amani, Gallawa amesema tunahitaji umoja na
mshikamano kuienzi amani na utulivu.
Hata hivyo amewataka wananchi
na jamii kwa ujumla kuanzia ngazi ya kaya, wazazi, walezi kuhakikisha
wanawajibika na kuzijua sheria za nchi sanjari na kuzitii ili kuitunza amani na
utulivu.
Hata hivyo ameupongeza Mkoa huo
kwa kua na Takwimu nzuri za uzalishaji.
Kwa upande wa viongozi wa
dini na viongozi kimila ambao waliwakilishwa na mwenyekiti wa machifu, Chifu
Nzunda pamoja na viongozi mbali mbali wa taasisi za serikali wakiwemo wabunge wamemuhakikishia Mkuu wa Mkoa huyo kua yupo katika jamii salama na
watashirikiana nae katika kuleta maendeleo ya Mkoa na Nchi kwa ujumla.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni