Salma
Said mwandishi wa DW Zanzibar ametoweka baada ya kutekwa na watu ambao
hawajafahamika jijini Dar es salaam, hali ambayo imeleta fadhaa na mshtuko kwa
waandishi, jamii na familia yake hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi
wa marejeo Zanzibar.
Ifahamike
kuwa Kazi ya mwandishi wa habari ni kutoa habari juu ya kila kinachoendelea
katika jamii , hivyo kama kuna dosari, dosari hiyo ni ya jamii na sio ya
anayeieleza dosari. UTPC inalaani na kupinga utekaji uliofanywa ambao sababu
zake bado hazijulikani, hivyo tunaitaka serikali kuhakikisha Salma Said
anatafutwa, kupatikana na anaachiwa huru mara moja kwa kuwa Serikali ndio yenye
jukumu la kulinda raia wake.
Kama
utekwaji wa Salma umefanywa kutokana na kazi yake ya uandishi habari tunalaani
vikali hatua hiyo, vitendo hivi havipaswi kuendelea katika nchi inayoheshimu
misingi haki na Demokrasia, Vitendo vya namna hii vinadumaza na kufifisha uhuru
wa habari .
Tunapinga
kwa nguvu zetu zote waandishi wa habari kukamatwa na vyombo vya dola au makundi
ya kihalifu kwa visingizio ama vya uchochezi au maslahi ya taifa. Waandishi
tutaendelea kufanya kazi zetu bila kujali vitisho vya aina yoyote ile kutoka
kwa mtu yoyote au Serikali.
Imetolewa
na
DEOGRATIUS
NSOKOLO RAIS WA KLABU ZA WAANDISHI WA
HABARI TANZANIA -UTPC.
March
19, 2016.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni