Wataalamu wanaohusika na matumizi ya
bangi kama dawa wanakutana Israel kujadili uvumbuzi zaidi katika kilichokuwakatika sekta yenye thamani ya mabilioni ya dola duniani.
Hayo
ndiyo maazimio ya Canna-Tech inayojumuisha wawekezaji, wakulima halali na
watumizi wa bangi kama dawa.
Uwekezaji
katika sekta hiyo umekuwa kwa kasi ya juu mno kufuatia kuhalalishwa kwa bangi
katika majimbo kadhaa nchini Marekani.
Nchini
Israeli sekta hiyo ya bangi halali imefunguka na inaelekea kukua kufuatia
utafiti na uwekezaji mkubwa.
Afisa
mmoja anayesimamia utafiti huo Saul Kaye anasema
''Wagonjwa
ni watu wanaopata matibabu ya maradhi ambayo yanapatikana baada ya kutumia
kemikali yenye madhara kama vile ugonjwa wa Saratani.
Watu hao ni wale
wanaougua ugonjwa wa kusahau, ugonjwa wa Crohn, na wale walio na msongo wa
mawazo au mfadhaiko.
Bangi
inaweza kusaidia matatizo kama hayo, na bado hatujajua manufaa mengine.
Utafiti
unahitajika zaidi, jambo ambalo Israeli inaendelea kuchunguza hasa katika ngazi
ya shirikisho
Kwa
sasa, kuna utafiti zaidi ya 36 unaoendelea katika hospitali nchini Israeli. ''
Biashara
hii ya bangi iliyoanzishwa kwa njia ya soko la magendo, na wafanyabiashara wa awali
walitokea hapo.
Lakini
kuna kampuni mahususi ya uundaji madawa, katika soko la hisa la Wall Street
Marekani sasa yanaangazia biashara ya bangi, hapo ndipo tunaivalia njuga, na
bila shaka tunaanza kubadili mtizamo kuhusiana na biashara ya bangi.'' alisema
Kaye.
Nchini Tanzania
mnamo February 2016, Mbunge wa Geita Vijijini kwa tiketi ya CCM, Joseph Kasheku
almaarufu kama Msukuma aliitaka serikali kufanya utafiti kisha kuidhinisha matumizi ya dawa za kulevya aina ya bhangi na mirungi
ili kuongeza pato la taifa kwa kupata fedha za kigeni,
Akichangia katika
bunge, Mbunge huyo alitetea kua bhangi husaidia kuongeza mzuka wa kufanya kazi
lakini imezuiwa huku serikali ikiruhusu viroba ambavyo watumiaji wake hushindwa
kufanya kazi baada ya kuvitumia,
“Mheshimiwa
mwenyekiti zao la mirungi na bhangi kuna nchi zinaruhusu. mfano mzuri ni
majirani zetu wa Kenya ambao ndege mbili kubwa hutua nchini humo kuchukua
mirungi na kupeleka ulaya. Sasa kwa nini sisi tusiendeleze zao hili linalopatikana
Geita na maeneo ya Bunda mkoani Mara na maeneo nchini ili wananchi wanufaike
kwa kuuza zao hilo?” alihoji
“kwa wasukuma kule
kwetu mtu akitumia bhangi anapata nguvu ya kulima sana hata hekari mbili lakini
inakatazwa na wakati huo huo vijana wetu tumewaruhusu kutumia viroba ambavyo
huwadhoofisha sana pengine kushinda hata bhangi, naomba tufanye utafiti upya
juu ya hili,”
Aidha aliendelea kwa
kusema “wapo wenzetu humu (wabunge) wanaitumia bhangi na hakuna madhara yoyote,
tena wanachangia hoja kwa ufasahakabisa,”
Hata hivyo hoja hiyo
ilipingwa na serikali, ambapo Naibu Waziri Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii,
Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Khamis Kigwangalla alieleza kuwa
madawa hayo ya kulevya yana madhara makubwa kwa binadamu. Hibyo serikali
haitaruhusu kwa namna yoyote matumizi yake kuyajadili
hata hivyo baada ya mbunge huyo kutoa hoja hiyo alizua gumzo kubwa katika bunge hata katika mitandao ya kijamii huku baadhi wakimtilia shaka kua huenda mbunge huyo ni miongoni mwa watumiaji wazuri wa mirungi aina ya bhangi, na wapo ambao alithubutu kusema mbunge huyo hajitambui
Mbunge wa Geita Vijijini kwa tiketi ya CCM, Joseph Kasheku almaarufu kama Msukuma |
wakati wa kampeni nchini Tanzania mwaka 2015, Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli ambae sasa ni Rais wa Tanzania, akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Geita vijijini Ndugu Joseph Kasheku (Msukuma) ambae sasa ni Mbunge wa Geita vijijini
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni