najua
unajiuliza mapacha si kawaida tu ?La hasha, Mapacha hawa imegunduliwa kuwa
walitungwa na baba wawili tofauti !
Taarifa
zinasema familia za mapacha hao iligundua kuwa watoto hawakufanana hata kidogo
hali ambayo iliwalazimu kufanyiwa
uchunguzi wa celi za DNA, na baada ya uchunguzi wa DNA, watoto hao walibainika
kuwa hawana uhusiano wa aina yeyote!
Taasisi
ya utafiti wa maumbile{ Genetic Association} inasema hali kama hii hufanyika
japo siyo kawaida na ni mara chache hali hiyo hutokea .
Taasisi hiyo imesema mwanamke anaweza kupata mapacha
na baba wawili tofauti ikiwa atajamiana na wanaume wawili katika kipindi cha
siku chache wakati ambapo mayai yake yameiva.
Kulingana
na profesa Dinh Luong, mtafiti mkuu wa taasisi ya utafiti wa seli na jeni
nchini Vietnam matokeo ya uchunguzi wa jeni ulibaini asilimia 100% kuwa watoto
hao hawakuwa wa baba mmoja.
''Inawezekana kuwa binti huyo alikuwa katika siku
ambayo mayai yake yalikuwa yameiva kwa kawaida mwanamke akiwa hapo anashikwa na
uchu kwa sababu mwili wake unatoa mayai na unataka mwanamume atakaye mpa
shahawa''
''kwa sasa tunaamini kuwa bibi huyo alilala na
wanaume wawili tofauti katika siku hiyo hiyo ambapo mayai yake yalikuwa tayari
na hivyo akatungwa mimba na wanaume wawili.''
''Hili linaweza kutokea ila ni tukio nadra sana''
alisema Profesa Luong.
''Kitaaluma kuna takriban wanawake 10 pekee duniani
ambao wamewahi kutungwa mimba na wanaume wawili kwa wakati mmoja.''
Kuna visa 10 pekee vya mapacha waliozaliwa na baba
tofauti duniani, huenda kuna hali kama hiyo lakini pengine wazazi huwa
hawaelewi, imeongeza taasisi hiyo.
Vyombo vya habari vya Vietnam vilianza kuripoti
kuhusu mapacha hao baada ya mmoja wa jamaa wao kusema pacha mmoja hakufanana
kabisa na mwenzake pia na wakiwemo wazazi.
Profesa huyo hakutaka kuendelea kuelezea kwa sababu
aliohofia angekiuka haki za mgonjwa wake na hata kuvunja ndoa.
Mapacha hao wa kipekee
waligonga vichwa vya habari kutokana na utofauti wao mkubwa na wazazi wao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni