Jeshi la Nigeria
limemkamata kiongozi wa kundi wapiganaji wa Kiislam la Ansaru lenye
uhusiano pia na kundi la kigaigi la Al Qaeda.taarifa ya msemaji wa jeshi
la Nigeria Brigedi Jenerali Rabe Abubakar inasema kuwa Khalid
al-Barnawi alikamatwa katika jimbo la Kogi nchini Humo.
Kukamatwa
kwa kiongozi huyo wa kundi la Ansaru tawi la Boko Haram kunafuatiwa
kusakwa kwa muda mrefu ambapo Marekani walitoa ahadi ya zawadi ya dola
millioni tano kwa yeyote atakayefanikisha kutiwa nguvuni Khalid al
Barnawi.
Ansaru ni kundi maarufu kwa utekaji wa raia kutoka nchi
za Magharibi na limekuwa likituhumiwa kwa mauaji ya raia kadhaa wa
kimagharibi pia.Brigedia Jenerali Rabe Abubakar amesema kuwa
kukamatwa kwa Barnawi ni hatua kubwa katika vita dhidi ya ugaidi.
“Ndiyo
tumemkamata gaidi.Yeah, kukamatwa kwake ni hatua kubwa katika vita
dhidi ya ugaidi,na si ndani ya Nigeria tu bali duniani kote".
kiongozi huyo alikua ni mtu
mhimu sana katika makundi ya mengi ya kigaidi Nigeria na Duniani,na tunajitahidi
kuhakikisha hatuishii kumkamata yeye tu bali na wengine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni