Ijumaa, 15 Aprili 2016

Imani potofu ni kikwazo katika juhudi ya kutokomeza mafonjwa yaliyokua hayapewi kipaumbele nchini!

Mratibu wa Taifa wa Magonjwa yaliyokua 
hayapewi kipaumbele Dr. Upendo John 
Mwingira, akifafanua jambo kwa 
waandishi wa habari
Waandishi wa Habari Mkoani Mbeya wakimsikiliza 
kwa umakini Mratibu wa Taifa wa Magonjwa 
yaliyokua hayapewi kipaumbele Dr. Upendo John Mwingira
Wizara ya afya imesema imani potofu ni changamoto katika kuzuia, kudhibiti na kutibu magonjwa yaliyokua hayapewi kipaumbele kama matende, mabusha, vikope,kichocho, minyoo ya tumbo na nk.

Haya yamesemwa na Mratibu wa Taifa wa Magonjwa yaliyokua hayapewi kipaumbele Dr. Upendo John Mwingira katika Semina ya siku moja ya Waandishi wa Habari  ya Magonjwa kumi na saba (17)ambayo yaliku hayapewi kipaumbele iliyofanyika katika katika Ukumbi  wa Hospital ya Mkoa Mbeya.

Dr Mwingira amesema imani potofu kama kurogwa, ni changamoto kubwa  katika wizara ya afya inayopelekea ugumu wa kutoa huduma ya matibabu kwa waathirika wa magonjwa hayo kama kichocho, vikope, matende, Usubi na mabusha kwa upande wa wanaume na wanawake ambapo alifafanua kua mabusha ya wanawake hufaamika kama vikokwa au vifigo.

Aidha amesema magonjwa hayo huambukiza kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine hivyo endapo mtu mmoja atakua nao katika familia kunauwezekano mkubwa wa kuwaambukiza wengine katika familia hali inayo pelekea familia moja kuwa na ugonjwa unaofanana na jambo hilo jamii huitafsiri kua ni kurogwa au kurithi jambo ambalo si kweli.

“unakuta katika familia moja baba, mama na watoto wanapata upofu ili hali walizaliwa wakima hawana upofu au karibia familia nzima inawagonjwa wa matende hivo jamii inayowazunguka inaona kama familia hiyo imerogwa na hata wanafamilia wenyewe huamini hivyo kumbe ni kwasababu ya kuto elewa chanzo cha upofu na chanzo matende na jinsi gani ugonjwa huo huambukizwa ” alisema dr. Upendo Mwingira

Aidha alitaja dalili za badhi ya magonjwa kama usubi ambapo mgonjwa hua na minyoo na dalili zake ni  kuvimba tumbo, kuharisha, kuumwa tumbo na kuongeza kua kwa asilimia kubwa ugonjwa huo unawashambulia zaidi watoto wadogo pamoja na ugonjwa wa vikope  ambapo dalili zake ni jicho kuwasha sana na mgonjwa hulazimika kujikuna na matokeo ni upofu.

Dr. Mwingira ameitaka jamii kuchukua hatua za makusudi mapema na kwenda kuwaona wataalamu wa masuala ya afya ili apatiwe matibabu mara tu anapo baini  dalili, lakini pia aameitaka jamii kuachana na imani potofu za kurogwa kwani ni hatari kwa mgonjwa na jamii inayomzunguka kwani baadhi jamii huamini kua ugonjwa wa abusha usababishwa na unywaji wa maji ya madafu jambo ambalo si kweli!

Dr. Mwingira amesema shirika la afya duniani WHO ikiwemo Tanzania imedhamiria kutokomeza magonjwa yote yaliyokua hayapewi kipaumbele ifikapo mwaka 2020!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni