Ikumbuke mnamo mwezi
February 2016 Bodi ya wakurugenzi wa magazeti ya Serikali,(TSN) ilimsimashisha
kazi Mhariri Mtendaji wa magazeti hayo Bw Gabrieli Nderumaki kupisha
uchunguzi kutokana na utendaji usioridhisha ndani ya kampuni hiyo.
Ambapo Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw
Prof Moses Warioba alisema hatua za kumsimamisha kazi Mhariri Mtendaji huyo zilitokana
na kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo hivyo
baada ya kumsimamisha nafasi yake ilichukuliwa na Naibu Mhariri Bi Tumma
Abdalah.
Sanjari na kumsimamisha kazi Mhariri huyo pia Prof Warioba alitengua
uteuzi wa Bw Felix Mushi aliyekuwa Meneja mauzo na masoko katika kiwanda cha
uzalishaji kwa kukosa sifa na utendaji mbovu uliopelekea kampuni kushuka katika
uzalishaji.
Hatua hiyo ya kuwawajibisha watendaji hao ilitokana na Ziara ya
Mhe. Nape Nnauye Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika
Kampuni hiyo ambapo Mh Nape pia hakuridhishwa na utendaji wa
watendaji hao uliopelekea wafanyakazi 21kuacha kazi.
“Nataka Bodi itafakari juu ya malalamiko yaliopo kwa wafanyakazi na
wachukue hatua kabla mimi sijakutana na wafanyakazi hao ili kujua mapungufu
yako wapi.”Alisema Mhe Nape.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea kampuni ya magazeti ya serikali TSN leo jijini Dar es Salaam. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni