Na Faraja Masinde, Dar Es Salaam
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Tumbi, David
Bundi, ameanguka kanisani na kuzirai wakati akimbatiza mtoto wa mchungaji
mwezake.
Tukio
hilo lilitokea jana wakati wa ibaada ya asubuhi katika Kanisa la KKKT
Usharika wa Kibwegere Kibamba, Dar es Salaam ambapo mchungaji huyo alikuwa
amealikwa na mchungaji wa kanisa hilo, Margret Chekoloa.
Mashuhuda
wa tukio hilo, waliokuwa kanisani hapo walisema kuwa, Bundi baada ya kumaliza
muda wa kusifu na kuabudu, ulifika wakati wa kubatiza, ambapo miongoni mwa
watoto waliokuwa wakibatizwa alikuwamo wa Mchungaji Margret.
“Kama
unavyojua kanisani tulikuwa tumemaliza utaratibu wa kusifu na kuabudu, kilikuwa
ni kipindi cha ubatizo na kati ya watoto waliokuwa wakibatizwa mmoja wapo ni
mtoto wa mchungaji wetu Grace Denis.
“Kitu
kilichotokea ni baada tu ya mchungaji kupiga magoti na mtoto huyo kwa ajili ya
kuanza kumbatiza alipoteza fahamu.
“Hali
hiyo ilizua taharuki kubwa miongoni mwa waumini wa kanisa hilo, hivyo ikabidi
awahishwe Hospitali ya Theofilo iliyoko Mbezi kwa Msuguri, na kuacha zoezi la
ubatizo likifanywa na mchungaji Margret ambaye alilazimika kumbatiza mtoto
wake,”.
Chanzo
hicho kiliendelea kueleza kuwa mara baada ya kufanyiwa vipimo kwenye hospitali
hiyo ilibainika kuwa mchungaji Bundi alikuwa na shinikizo la damu (presha)
ambayo ilifikia 211 na hivyo kulazimika kuongezewa maji.
Kwa
upande wa Mchungaji hakua tayari kuelezea tukio hilo badala yake alitaka
watafutwe baadhi ya waumini wanao abudu kanisani hapo ili waweze kuzungunzia
tukio hilo.
“Siwezi
kuongelea tukio hili, naomba uwatafute waumini wengine wa kanisa hili watakupa
taarifa ila kwangu inakuwa ngumu kukwambia,” alisema Mchungaji Margret.
Waumini
wa kanisa hilo walisema kuwa hilo ni tukio la kwanza kutokea kanisani
hapo, liliwapa wakati mgumu na kujikuta wakitoka nje kwa taharuki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni