Mtuhumiwa wa kesi ya kumtukana Rais John Pombe Magufuli katika mtandao, Isaac Emire (katikati) akiongozwa na askari kuelekea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kujibu mashtaka ya kesi hiyo |
Mkazi
wa Olasiti Jijini Arusha, Isaac Emily (40), amepandishwa kizimbani kwa kumtolea
maneno ya dharau na kumdhihaki Rais John Magufuli katika mitandao ya kijamii.
Bw. Emily alisomewa
mashitaka jana na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Gaudencia Masanja mbele ya
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Augustino Rwezile, katika mshitaka Emily anatuhumiwa kutenda kosa la kutoa lugha ya matusi dhidi ya Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli Machi 17
mwaka huu kinyume na sheria ya mitandao namba 16 kifungu namba 14 ya mwaka
2014.
Masanja
alidai kuwa, siku hiyo mshitakiwa alisambaza ujumbe wa uongo katika mitandao ya
kijamii wenye lengo la kumdharau, kumdhihaki na kumtolea maneno Rais Magufuli kwa
lengo la kumdhalilisha.
Mtuhumiwa Emily anadaiwa kuandika ujumbe uliosomeka ”Hizi ni siasa za maigizo halafu mnamfananisha
huyu bwege na Nyerere wapi bwana.’’
Mshitakiwa
huyo alikana kutenda kosa hilo ambapo Mwendesha Mashitaka aliomba Mahakama
isitoe dhamana kwa mshitakiwa huyo, kwa maelezo kuwa ingawa dhamana ni haki
yake ya msingi, lakini usalama wake utakuwa shakani kwani watu wengi wamekerwa
na ujumbe huo na pia akiwa nje anaweza kuvuruga ushahidi.
Hata hivyo, Emily
hakukubaliana na madai ya Mwendesha Mashitaka na kusema ana uhakika hataingilia
upelelezi wa kesi hiyo kwa sababu simu zake zote ziko mikononi mwa Polisi,
hivyo madai ya kusema ataingilia upelelezi si ya kweli.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni