Na.Catherine Sungura,kahama
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiangalia kifaa cha kutengenezea maji tiba kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa shinyanga |
Waziri wa afya Mh.Ummy Mwalimu akiongea na baadhi ya wakazi wa kahama waliofika hospitalini hapo kuangalia wagonjwa wao |
Waziri.Ummy Mwalimu akitoa maelekezo kwa wagonjwa waliofika kupata matibabu kwenye Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga |
Mh.Ummy Mwalimu akiwaelekeza kamati ya afya ya wilaya ya kahama mahali linapotakiwa kuwekwa bango linaonesha huduma za wazee inapopatikana |
Mfamasia mkuu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa shinyanga Luciano Lodrick akimpatia maelezo waziri wa Afya, Ummy Mwalimu jinsi ya utengenezaji wa maji tiba |
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh.Vita Kawawa(Katikati) akionesha kwa vitendo bango hilo linapotakiwa kuwekwa, kushoto ni Mh.Ummy Mwalimu na kulia ni mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Kahama Anderson Msumba |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Kahama amepewa siku tisini awe
amenunua mashine ya mionzi (x ray)kwa ajili ya hospitali ya mji kahama.
Agizo hilo amepewa jana na Waziri wa Afya,maendeleo ya
jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu wakati alipotembelea hospitali hiyo
pamoja na kuongea na watumishi wa kada ya afya wa mji huo.
Waziri Ummy alisema ametoa agizo hilo ili kuweza kurahisisha
usumbufu wanaopata wananchi wa wilaya hiyo kwa kwenda kupata huduma nje ya
hospitali ambapo wakati mwingine vipimo hivyo vinakuwa havisomeki vizuri kwa
kukosa viwango vinavyo stahili za mashine hizo.
Hata hivyo waziri ummy alisema upatikanaji wa mashine hizo utapunguza
malalamiko mengi toka kwa wananchi kwa ukosefu wa kifaa tiba hicho kwani hospitali
hiyo hivi sasa inahudumia wananchi zaidi ya milioni moja hususan toka wilaya
zote.
Aidha, alizitaka halmashauri zote mjini kuweza kuwekeza kwenye
huduma za vifaa tiba ambavyo vinarahisisha kugundua matatizo yanayowakabili
wananchi wanaofika kwenye kupata huduma na hivyo kuwapatia matibabu stahili
wagonjwa wanaofika kupata matibabu kwenye vituo vya kutolea huduma nchini.
“siku hizi lazima muwekeze
kwenye kununua vifaa tiba ili kuweza kupata kutoa huduma nzuri, pesa mnakusanya
na kahama ni halmashauri tajiri, mkurugenzi nakupa siku tisini uwe umenunua
mashine hiyo”
Naye mkuu wa Wilaya hiyo
Mh. Vita Kawawa amemuahidi waziri huyo kwamba amepokea maagizo yote aliyoyatoa
na atayafuatilia ili kuweza kutatua malalamiko ya wananchi na yale ya watumishi
wa kada ya afya
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni