Ijumaa, 15 Aprili 2016

Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla amezifungia hospital mbili tofauti zinazomilikiwa na Raia wa kigeni

Naibu Waziri Dk. Kigwangalla akikagua moja ya lesini
Naibu waziri akikagua moja ya dawa ambazo ni hatari kwa binadamu 
Kitanda kilichokutwa kikitumika kutolea huduma za kitabibu kinyume na utaratibu

wakorea ndiyo waliokutwa ambapo wamebainisha kuwa wao wanatibu magonjwa ya ngozi pekee yake lakini uchunguzi unaonyesha wanafanya na operesheni


Baadhi ya vifaa vilivyokutwa hospitalini hapo

Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla amezifungia hospital mbili tofauti zinazomilikiwa na Raia wa kigeni wakiwemo kutoka Korea kwa kile walichoeleza kuendesha huduma hiyo bila vibali maalum ikiwemo usajiri wa msajiri wa hospital binafsi pamoja na ule wa msajiri wa tiba mbadala.

Hospital hizo zilizovamiwa na kukaguliwa ni pamoja na Korea Medical clinic (Kariakoo) Mtaa WA Mahiwa na nyingine ni Oriental Traditional medicine clinic. Ambazo zote zinazomilikiwa na Mabong.

Dk. Kigwangalla ameeleza kuwa watu hao wamekuwa wakitoa huduma bila vibali halali huku pia wakiendesha huduma pasipo kufahamu lugha za kiswahili na Kiingereza

Hata hivyo katika ziara hiyo Kigwangalla alibaini uwepo wa vifaa vile vinavyotumika mahospitalini na miongoni mwa vifaa hivyo ni vile ambavyo hawakuruhusiwa kuvitumia hospitalini hapo.

Hata hivyo baada ya ukaguzi huo ilibainika kua wakorea hao wamekua wakitoa huduma za upasuaji ili hali hawana kibali cha kutoa huduma hiyo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni