Rais Magufuli akikata utepe kuashiria daraja limezunduliwa rasmi |
Rais Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Wilson
Kabwe kutokana na tuhuma za ufisadi katika utekelezwaji wa mikataba mitatu, inayohusu maeneo ya
ukusanyaji mapato ya Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo Mikoani ya Ubungo na kodi ya
uegeshaji magari katikati ya mji na kuisababishia
serikali hasara ya bilioni 3.
Rais Magufuli amechukua uamuzi huo wakati
wa uzinduzi wa daraja la Kigamboni, ambapo kabla ya Rais kuhutubia, Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alitoa Hotuba fupi ya maswala kadhaa
ya Mkoa wa Dar es Salaam ikiwemo ripoti ya tume aliyounda
kuchunguza utekelezwaji wa mikataba hiyo.
Katika hotuba hiyo, Makonda alisema,
Kamati aliyounda ilibaini kuwa pale ubungo kunatumika sheria ndogo mbili
za ukusanyaji mapato moja ya mwaka 2004 na nyingine ya mwaka 2009 ambazo
zote zilisainiwa na Wilson Kabwe.
Amesema kuwa Sheria ya
Mwaka 2004 ya ukusanyaji mapato, inaonesha kuwa kila basi linaloingia
Ubungo linatakiwa kutozwa Sh 4,000, hivyo makusanyo halisi kwa mwezi ni Sh
milioni 42 kutokana na mabasi 350 yanayoegeshwa kituoni hapo
na Sheria ya Mwaka 2009 ya ukusanyaji mapato, inaonesha kuwa
kila basi linaloingia Ubungo linatakiwa kutozwa Sh 8,000, hivyo makusanyo
halisi kwa mwezi ni Sh milioni 82 kwa mwezi
Makonda amesema kwamba, Kabwe alisaini
mikataba miwili, wa 2004 na wa mwaka 2009 ambapo ule wa mwaka 2004
ulipelekwa jiji na ule wa 2009
ukapelekwa kwa mzabuni, hivyo
jiji wanajua kuwa basi linatozwa sh. 4000 kwa siku wakati mzabuni anatozwa 8000 kwa siku
Kutokana na maelezo hayo,
Mheshimiwa Rais akatangaza kumsimamisha kazi bwana Kabwe ambaye ni
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam na ameagiza vyombo vya dola vianze
uchunguzi mara moja ili hatua zaidi za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya
mkurugenzi huyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni