Jumatano, 20 Aprili 2016

Mwalimu Mkuu Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya amefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumpachika mimba mwanafunzi wake wa darasa la saba.

Na Frederick siwale mbarali mbeya

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Utyego iliyopo katika Kata ya Ubaruku Wilaya ya Mbarali mkoani mbeya, amefikishwa mahakamani hii leo kwa tuhuma za kumpa mimba mwanafunzi wake.

Mtuhumiwa Shusha M Wameambiwa (45) ambaye ni Mwalimu mkuu wa shule hiyo, amepandishwa kizimbani mbele ya hakimu mafawidhi wa mahakama ya Wilaya ya mbarali Agenesi Ringo kwa tuhuma za kupatia mimba mwanafunzi wake wa darasa la saba a (jina lake linahifadhiwa)  nayesoma katika shule hiyo ya Utyego.

Akizungumza na muandishi  mahakamani hapo afisa Ustawi wa Jamii Wilaya Winfrida mahali, amesema kitendo alichofanya mtuhumiwa ni ukatiri wa kijinsia. 

Naye afisa ustawi wa Jamii anayeshughulikia kitengo cha mahakama David Makele, amesema vipimo vya madaktari vinaonyesha kuwa ujauzito huo una umri wa miezi nane na nusu.

Aidha mkurugenzi wa shirika la kupinga ukatili dhidi ya watoto na Wanawake Tanzania (SHIKUMWATA) Leopard Kitalima, amesema Wilaya hiyo inakabiliwa na wimbi kubwa la Vitendo vya ukatili na unyanyasaji kwa watoto na Wanawake na kudai kuwa changa moto kubwa ni kukosekana kwa elimu ya sheria na haki kwa jamii.

Mashitakiwa mwampamba yupo nje kwa dhamana hadi mei 5 mwaka huu kesi hiyo itakapoletwa tena.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni