Ndugu waandishi wa Habari, wanaharakati na watanzania wote.
Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na
Uhalifu Tanzania (OJADACT). Tunalaani vikali kuzuiwa kwa Waandishi kuingia
Bungeni kwa lengo la kufanya coverage ya vikao vya Bunge la kujadili mpango wa
maendeleo ya miaka mitano na bajeti ya serikali.
OJADACT, hatukubaliani na utaratibu wa sasa wa kutumia idara ya
habari na maelezo ya Bunge, kuwa ndio wenye jukumu la kukusanya taarifa na
kuzigawa kwa waandishi.
Ni ukweli usiopingika kuwa, maamuzi hayo yana athari zifuatazo.
Kuminya uhuru wa haki ya kupata taarifa kwa wananchi kama
ilivyoainishwa kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 18.
Kuminya uhuru wa vyombo vya habari, ambao umekuwa ukikosa haki ya msingi
iliyokosekana kwenye Katiba.
MSIMAMO WETU.
1: Kwa kuwa Bunge halioni umuhimu wa waandishi Bungeni basi
tunaviomba vyombo vyote vya habari vya binafsi kuwatoa waandishi wao bungeni.
Tunaviomba vyombo vyote vya habari vya binafsi kususia kuandika habari za bunge
hadi hapo litakapotengua utaratibu huo.
Waziri mwenye dhamana ya
habari afute kauli yake ya kejeli kuwa wanaopinga utaratibu huo eti waende
Mahakamani.
Ahsanteni sana wanahabari kwa kuitikia wito wetu.
Edwin Soko Mwenyekiti
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni