Kocha wa timu hiyo ambaye pia Mbunge
Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Mh. Venance Mwamotto (kati) akitoa maelekezo katika mazoezi hayo.
|
Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Mh. Steven Ngonyani ‘Maji Marefu’ akisimamia mazoezi hayo kwa muda asubuhi ya leo |
*****************************
Timu ya Bunge Sports Club kucheza na timu ya Baraza la
Wawakilishi Zanzibar kesho Aprili 26 saa 12 Jioni
Timu ya Mpira wa miguu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano la
Tanzania Bunge Sports Club inatarajiwa kushuka dimbani kucheza mchezo mkali na
wa aina yake ambao ni wa kwanza na timu ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar.
Mapema leo Aprili 25.2016 timu hiyo ilishuka katika dimba hilo
la Amaan Studium na kupasha misuli maalum kwa mchezo huo wa kesho ambapo kwa mujibu wa
viongozi wa timu hiyo ya Bunge wametamba kuibuka na ushindi wa kishindo.
Kocha wa timu hiyo ambaye pia Mbunge Jimbo la Kilolo mkoani
Iringa, Mh. Venance Mwamotto ametamba kwa timu yake kuibuka na ushindi mnono
katika mchezo huo kwani wana mazoezi ya kutosha na pia wamejiandaa kuonyesha
uwezo.
“Tunawaomba wabunge wote
kutuunga mkono katika mchezo huu kwani timu imejindaa vya kutosha kuhakikisha
tunashinda. Mchezo huu ni maalum kwa ajiri ya kuimalisha Muungano wetu tukufu
hivyo tutaendelea kuuenzi na kuukumbatia na sote kwa pamoja tuzidishe Amani”
alieleza Mh. Mwamotto.
Kwa upande wake Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Mh. Steven
Ngonyani 'Maji Marefu' ambaye ni miongoni mwa viongozi wa msafara wa timu hiyo
ya Bunge ametamba timu yake kuibuka na ushindi mnono kwani wamejiandaa
kisaikolojia na mazoezi ya kimichezo.
Naye Mbunge wa Nzega Vijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla ambae
ni miongoni mwa viongozi wa timu hiyo ya Bunge amebainisha kuwa, mchezo huo
unatarajiwa kuchezwa majira ya Saa 12 Jioni kesho Aprili 26.2016 katika uwanja wa
Amaan uliopo Unguja.
“Mechi kati ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. Utachezwa kesho ni siku ya
Kuadhimisha Muungano wa Nchi ya Jamhuri ya Tanganyika Na Jamhuri ya Watu wa
Zanzibar. Tunawaomba watu kujitokeza kwa wingi kuuona mchezo huu ambao utakuwa
wa aina yake kwa timu zote mbili.” Alieleza DK. Kigwangalla.
Timu hiyo ya Bunge yenye
wachezaji Zaidi ya 19 imejiandaa vya kutosha katika kuhakikisha inapata ushindi
mnono na ipo Visiwani Zanzibar kwa maandalizi ya mchezo huo tokea jana na leo
imeweza kufanya mazoezi ya awali asubuhi na mengine wakitarajia kufanya hapo
jioni!
Benchi la ufundi likiwa tayari katika mazoezi hayo |
Mazoezi ya timu ya Wabunge yakiendelea katika uwanja wa Amaan Stadium, Unguja leo Aaprili 25.2016. |
Mazoezi yakiendelea |
Mbunge wa Nzega Vijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akionesha uwezo wake katika mazoezi hayo |
(Picha zote na Andrew Chale-Zanzibar)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni