Ijumaa, 8 Aprili 2016

Watu 13 wapoteza maisha baada ya kuangukiwa na nyumba, kufuatia mvua kali zilizo nyesha siku 4 mfululizo,

Habari na Ephraim Mkali-Malawi.







Wakati ambapo nchi ya Malawi ina kumbwa na janga la njaa simanzi zimetawala mjini Mzuzu baada ya watu kumi na tatu kufariki dunia kutokana na kuangukiwa na nyumba zao walizokua wakiishi.

 Ni siku ya nne mvua zimekua zikinyesha mfululizo katika muji wa Mzuzu, tarifa kutoka katika hosipitali ya rufaa ya mjini Mzuzu imekua ikipokea mamia ya watu walio pata majehuri,

Mamlaka ya hali ya hewa nchini Malawi ili onya kuwepo kwa mvua kubwa mwezi huu, hata hivyo mamlaka hiyo imetahadharisha kua kuna uwezekano mkubwa idadi ya watu hao ikaongezeka,

kikosi cha jeshi la Malawi kime ungana na jamii kuokoa watu katika maeneo ambayo  yameathiriwa zaidi na janga hilo,
tutaendelea kukujuza wasomaji wetu yatakayo jiri zaidi huko nchini Malawi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni