Jumatatu, 18 Aprili 2016

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na Waziri wa kilimo na mifugo Mwigulu Nchemba wafungua Machinjio ya Vingunguti,

Matukio mbali mbali katika picha ufunguzi wa machinjio ya vingunguti jijini Dar Es Salaam

Mkurugenzi wa manispaa ya ilala Isaya Mgulumi(mwenye miwani) akiwaeleza mawaziri wa wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto,Ummy Mwalimu(katikati) na waziri wa kilimo na mifugo, Mwigulu Nchemba(kushoto) akiwaelezea hali ya ukarabati wa machinjio hayo
Mbunge wa jimbo la segerea Bona Kalua,akiongea na wanachama wa Umoja wa Wafanyabiasha wa ng'ombe na mazao yake(UWAMI) kwenye mkutano wa pamoja na mawaziri hao
Mkaguzi toka TFDA dkt. Mwanga Itikija(mwenye shati la pink)akiwaonesha mawaziri hao eneo ambalo lilikua likiuzia nyama kwa reja reja kinyume na kanuni ya afya

Waziri Mwigulu Nchemba akiongea na Umoja huo na kuwapatia siku tatu ili waendelee na uchinjaji wa ng'ombe walizonazo na baada ya hapo wataendelea na ukarabati wakati huo machinjio ya mazizini yatakua yamekamilisha ukarabati na kufunguliwa.
Mawaziri Ummy Mwalimu na Mwigulu Nchemba wakisoma vielelezo vilivyowasilishwa na diwani wa kata hiyo


Naibu Meya wa manispaa ya ilaya ambaye ndio Diwani wa kata ya vingunguti Omary Kumbilamoto akiongea kwenye mkutano huo

Wanachama wa Umoja wa wafanyabiashara hao waliwasikikiliza mawaziri hao
Baadhi ya wafanyabiashara wa machinjio hayo wakifuatilia ziara hiyo
(Picha na Wizara ya Afya)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni