Na.Catherine
Sungura,Msalala
wakina mama wanao jishuhulisha na kazi ya kuponda kokoto karibu na kituo cha afya kinachojengwa katika kata ya Bugarama Halmashauri ya Msalala wilayani kahama. |
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu upande kulia akizungumza na mmoja wa akina mama wanaoponda kokoto katika kata ya Bugarama Halmashauri ya Msalala wilayani kahama. |
Waziri Ummy Mwalimu akikagua ujenzi wa kituo cha afya kilichopo kata ya Bugarama. |
Muonekano wa kituo hicho cha Afya kilichopo katika kata ya Bugarama ambacho ujenzi wake bado haujakamilika. |
Waziri Ummy Mwalimu akimsalimia mlemavu kata ya Bugarama |
Mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala wilayani Kahama, amepewa
wiki mbili awe amempatia ripoti waziri wa afya, Ummy Mwalimu, kuhusu wanawake
wanaoponda kokoto wamewezeshwa kwa kupatiwa mkopo wa kiasi gani na mafunzo
yapi.
Waziri Ummy
Mwalimu ametoa agizo hilo baada ya kufika katika halmashauri hiyo kukagua
ujenzi wa kituo cha afya kilichopo kata ya Bugarama kinachojengwa na kampuni ya
mgodi wa ACACIA iliopo Bulyahulu na kuwakuta wanawake mbele ya majengo hayo
wakiponda kokoto kwa kutumia vifaa duni na vya mkono.
Waziri Ummy
alisema hivi sasa kuna vitendea kazi vya Kisasa na vya bei rahisi ambayo
vitawasaidia wanawake hao kuwarahisishia
wanawake kuacha
kushinda masaa kumi wakiponda mawe
"Baada ya
makusanyo ya Mapato ya ndani,mkurugenzi unatakiwa kutenga asilimia 5 kwa ajili
ya vikundi vya akina mama na sio vikundi vya kujitafutiza huko mitaani na vya
kujuana"
Waziri Ummy
alisema haiwezekani wanawake wanaojishughulisha na shughuli ndogondogo
wakaachwa pasipo kusaidiwa kwani wanawake wengi ndio wanaosaidia familia.
"Tusipowawezesha
wanawake hawa,mnataka tuwawezeshe wanawake gani? hawa ndio waliotupigia kura
hawa, lazima tuwaoneshe maneno ya Rais Magufuli hayakuwa matupu maana alisema
anataka kuwawezesha wanawake na ndio maana kila halmashauri inatakiwa kutenga
asilimia kumi ya mapato yake kwa ajili hiyo"
Aidha,alisema
wawahamasishe wanawake wengine katika Kata zote kujiunga kwenye vikundi hususan
wale wanaojituma na kujitoa kwa biashara ndogondogo,
Wanawake hao
wapatao thelathini wanaoponda kokoto karibu na kituo cha afya Bugarama walisema
wanaomba wanawake wawezeshwe kwani hawajui kama kuna pesa zinatakiwa kutengwa
kwa ajili ya wanawake, hata hivyo walimshukuru waziri huyo kwa kuwafumbua
macho.
Naye mganga mkuu
wa halmashauri hiyo dkt. Hamad Nyembea alisema kampuni hiyo ya ACACIA ilianza
ujenzi wa kituo cha afya julai,2014 na hadi kukamilika ujenzi huo itagharimu
zaidi ya shilingi bilioni 1.7, na ujenzi wa zahanati ya Bulyahulu utagharimu
zaidi ya milioni mia tatu!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni