Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Mh. Nape Nnauye akimpongoza, Katibu Mkuu wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya baada ya kuwasilisha Risala. |
Baadhi ya wadau wa sekta ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo wakimsikiliza kwa umakini Waziri wa Nape Nnauye wakati akitolea ufafanuzi baadhi ya changamoto zilizowasilishwa kupitia Risala |
Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Mh. Nape Nnauye amewataka wana Mbeya kuikataa siasa katika michezo
Nape amesema hayo wakati
akizungumza na wadau wa Tasnia Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, viongozi wa
serikali pamoja na taasisi mbali mbali mkoani Mbeya walio hudhuria katika ziara yake
hii leo katika ukumbi wa Mkapa uliopo Sokomatola Mkoani Mbeya.
Nape amesema kua siasa ni adui
mkubwa anaekwamisha mikakati katika tasnia ya Michezo nchini huku akitolea mfano
timu ya Mbeya City Fc ambayo kwa sasa inaonekana kutofanya vizuri kutokana na
kuingiza siasa,
Aidha amewataka viongozi na
mashabiki wa michezo kuitumia vizuri Timu ya Mbeya City Fc na timu nyingine
zilizopo mkoani hapa katika kuiunganisha jamii pamoja badala ya kuwagawa,
Hata hivo amewakemea viongozi
ambao wamekua akiingiza masuala ya siasa katika timu hiyo kwani Mbeya City
Fc inaendeshwa kwa kutumia pesa za jiji ambazo ni pesa za umma na kuongeza kua katika
uchangiaji wa fedha hizo hakuna anaeulizwa chama hivyo hakuna chama chochote
chenye dhamana ya kuifanya timu hiyo iwe chini yake.
Ameongeza kua wizara yake ya
Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo ni wizara yenye wadau wengi zaidi na ndiyo wizara
isiyo na itifaki, amesema kufuatia changamoto ambazo zinaikabili sekta ya
michezo Serikali imeamua kufanya
marekebisha sheria ili iendane na sera ya michezo lengo ni kuifanya michezo kua
shughuli rasmi ya kiuchumi na kwamba zoezi hilo lipo katika hatua za mwisho kukamilika.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Mbeya mh.
Amosi Makala amemuahidi Waziri kua atahakikisha anasimamia kwa umakini mkubwa sambamba na anaondoa
kero ya siasa katika michezo,
Kwa upande wa wadau wa
michezo mkoani Mbeya wamesema ili kuondoa kero ya Siasa viongozi wanapaswa
kuheshimu taratibu zilizowekwa pindi wanapo hudhuria katika mechi ikiwa ni
pamoja na kukaa katika sehemu wanazo stahili, kwani kumekua na tabia ya baadhi
ya viongozi mbali mbali wakiwemo wana siasa kuto kaa sehemu rasmi walizo
andaliwa badala yake huenda kukaa kwa mashabiki jambo ambalo linachangia
kuingiza siasa katika michezo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni