Ijumaa, 22 Aprili 2016

Yericko Nyerere apondwa na wadau wake mtandaoni kisa kuifananisha Bangi na Sakramenti katika maelezo yake mwenyewe amesema leo ni siku ya BANGI DUNIANI


Leo ni siku ya wavuta bangi duniani,
Marastafari wenzangu popote mlipo tuitumie siku hii kuelezea na kuwafunza watu umuhimu wa sakramenti ya bangi kwa dini yetu ya Rastafariani.
Tupinge matumizi holela ya sakramenti hii kwani ni imani takatifu kwetu, tuivute pindi tutakapotaka kuzungumza na Jah wetu tu.
Tuungane na serikali kukomesha matumizi holela ya bangi kwa vijana nchini, katika kitabu kitakatifu kwa Wakristu kiitwacho BIBLIA tunasoma yakuwa, "nd I will raise up for them a plant of renown, and they shall be no more consumed with hunger in the land, neither bear the shame of the heathen any more". -- Ezekiel 34:29
Maana halisi ya RASTAFARIAN ni imani ya mtu mweusi au mweupe inayotetea UTU wa MTU MWEUSI. MPIGANIA HAKI YA MTU MWEUSI huitwa RASTAMAN au RASTAWOMAN na kwa WATOTO wao huitwa RASTABABY.
Imani "kamili" ya Rasta ilianzishwa zaidi ya miaka 100 iliyopita huku kundi kubwa la waafrika waliokuwa mikononi mwa wakoloni walipoweza kuingia kwenye imani hiyo huku nchi ya JAMAICA ikiwa na wafuasi wengi. Dredy locks ni moja kati ya kitambulisho kikubwa cha Rastafarian,,lakini si kila mwenye dredy locks basi akawa Rastafarian kwani asilimia 25 ya Rastafarian hawana Dredy locks na ndipo tunapoona kwamba kufuga dredy si kuwa na imani ya Rasta bali matendo humpeleka mtu kwenye imani ya Rasta. Rastaman hupenda kujiajiri na mara nyingi hufanya shuhguli zake kwa kutumia mikono na si vifaa vya kazi na kati ya kazi za Rasta ni SANAA, wao hufanya aina zote za sanaa lakini kazi zote hizi Rasta hujiajiri na si kuajiriwa.
Moja kati ya nguzo kuu za Rastafari ni UPENDO na AMANI, Rasta hujaribu kutafuta amani popote ipatikanapo, tabia hiyo ya Rasta imewafanya Rasta kuheshimiwa popote pale waingiapo lakini baadhi ya jamii huwa tofauti na imani hii.
Imani ya Rasta chimbuko la asili ni Nimrodi binadamu wa kwanza mweusi na mtawala wa Babeli ya kale, na kutukia kwake kumechipuza kamili nyakati ambapo haki ya mtu mweusi ilipo potea na hatimaye jamii kubwa ya watu weusi kutafuta njia ya kutetea utu huo wa mtu mweusi.
GABRIEL HAIRE SELASIE aliyekuwa kiongozi wa nchi ya Ethiopia ni moja kati ya watu waliochangia kukuza imani ya Rasta ulimwenguni na ndipo jumuiya ya Rastafariani ilipoamua kumteua kuwa kiongozi wa Rastafarian ulimwenguni.
Rasta hutumia muda wa mapumziko kwa kusikiliza burudani ya nyimbo za rege walizo zitunga ambazo nyingi ya nyimbo hizo huwa za kuwapa moyo na kuwafariji watu wanyonge na wanaopuuzwa.
Rege kwangu nisehemu ya Ibada ya kweli ambapo hutumia mziki huo siku za jumamosi kama sehemu ya kuwasiliana na Mungu wangu, Hakika Mungu hunijibu tena LIVE.
Labda nipende kusema kuwa watu wengi wanafikiri kuwa Rastafari ni kuvuta Bangi na kuwa na dreads (Dreads ni muhimu).
Kuwa Rastafari nilazima uishi nakufuata yafuatayo:
Fuata sheria za Nazareti katika Bible(Rastafarian Bible).
Epuka vyakula najisi kama nguruwe, kambale n.k
Epuka intoxicants kama pombe, sigara, kahawa, coca cola na vyakula ambavyo sio natural na vyenye madhara mwilini.
Heshimu utamaduni wa Africa na kubali kuwa wanadamu wote asili yetu ni Africa na ndio Zion Yetu
MHESHIMU KING OF KINGS, THE LION OF JUDAH, ELECT OF GOD, RAS TAFARI MAKONEN, HAILE SELASSIE, THE POWER OF THE TRINITY, KING MESIAH FROM THE ROOT OF KING DAVID IN A SOLOMONIC LINEAGE.
Kuwa msafi, usimuudhi mtu, Heshimu imani za watu, usibague mtu kwa kuangalia imani, kabila wala rangi.
Jali Elimu kwa kuwa ndio msingi wa Haile kujikomboa.
Heshimu mother nature na usiharibu mazingira.
Usiue mnyama wala kumpiga bila sababu.
Heshimu dini/imani za watu wengine,
Tambua uwepo wa Yesu Kristu na Mtume Mohamed SAW (japo mafundisho yao usiyafue)
Epuka kugusa damu wala kunywa damu.
Heshimu Bendera ya Empire ya Ethipia na Rasta colour, usivae ovyo kama urembo,
Jali equality, kuwa natural na epuka vitu vya kemikali n.k
Tafari Makomein (Gabriel Haile Selassie) ni God incarnate.
Pengine hili swala la kumwabudu Haile Selassie limebaki kwa " Root Rastafarians" yaani mimi na wale walio devote maisha yao yote katika namna ya asili ya Rastafari.
Maisha yanabadilika halikadhalika mawazo na mitazamo pia.
Rastafari sasa inaonekana kuwa kama lifestyle na pengine ni jambo jema. Kuwa Rastafari kama Kebra(Rastafari Holy Book) inavyosema ni kuwa na namna ya maisha yaliyo nyofu.
Hii inatia ndani; upendo, heshima, na amani. Kwa Rastas tunasema " don't haffi dreadlocks to be rasta, a Rastaman is a conception of the heart"
Kaya ni "sakramenti" kwa maana ya kwamba inatumiwa wakati wa worshipping kwa dhumuni la ku "calm yourself" na kutafuta oneness na muumba "Jah".
Ikumbukwe kwamba, Rastafari sio organized religion lakini ni imani yenye tumaini tofauti na inabeba mafundisho mengi ya bible hasa old testament.
Hauitaji kuacha kazi, dini yako, mke wako/mume au umkane mtu fulani ili uwe rasta. Kuwa rasta ni kuishi maisha bora kama nilivyo taja hapo huu.
Mpende mzazi wako, jali utu wa mwanadamu na viumbe vingine hapo utakuwa Rastafari kwa matendo. Kuhusu ku "smoke Kaya" ni uamuzi japo wengi tunatumia.
Kuwa rastafari ni very hard, inabidi uwe makini na ukubali kupata chalenges nyingi za maisha na watu kukuhukumu kwa kukuangalia na wengine kukuona mjinga. Ila ni raha sana kwa kuwa utaishi maisha ya furaha bila kujali what they think.
BLESSINGS!


Mara baada ya kupost ujumbe huo hapo juu baadhi ya mashabiki wake waka comment kama ifuatavyo!
Comments
Richard Maliwanga Umesharanduka!!
Like · Reply · 1 · 1 hr
Samwel Shamy Umerukwa na akili eee
Like · Reply · 1 · 1 hr
Prosper Juma Ahaaaa....kuumbeeee.....daah....nilikuwa najiuliza hiv hiz tabia za kuzusha mambo umezitoa wap...aah..kuuumbeeee
Like · Reply · 1 · 1 hr
Haidar Ally hii kali bangi nayo ina cku
Like · Reply · 1 · 1 hr

Erick Moshi Please explain to me una maana gani unapo sema matumizi holela
Like · Reply · 1 · 1 hr
Elias Peter Mwanangwa Bangi unafananisha Na sakramenti?ndo naanza kukuelewa kuwa ww si mzima kabisa huwezi kufananisha upuuzi Na sakaramenti,ninachoamini kwa sasa Ni kuwa unatafta umarufu wa kijinga kabsa
Like · Reply · 3 · 1 hr
Petronila Thomas Mteu Rasta wote wanaita bangi sacrament....
Like · Reply · 50 mins

Rosemary Adriano mmmmmh jaman dunian ina mambo shereh inafanyika wap kitaifa
Like · Reply · 2 · 1 hr
Mungiki Kangayas Pamoja sana
Like · Reply · 22 mins
a reply...

Conrad Mc Yericko saman nipo nje ya mada ivi kimsing ukimaliza chuo unatakiwa ukae mda gani upewe vyeti vyako
Like · Reply · 1 · 1 hr
=
Mwl Egno Wa Ndwango nd I will raise up for them a plant of renown, and they shall be no more consumed with hunger in the land, neither bear the shame of the heathen any more. -- Ezekiel 34:29
Like · Reply · 1 · 1 hr
Yericko Nyerere Elias Peter Mwanangwa umeielewa mada hii kweli au umekurupuka tu? Tuliza moyo na akili kisha usome tena na tena
Like · Reply · 1 · 1 hr

Elias Peter Mwanangwa Sakaramenti takatifu uilinganishe Na Bangi?sijakurupuka Ni vitabu gani vitakatifu vinavyoelezea juu ya hizo sakramenti aina bangi?
Like · Reply · 57 mins

William Miyungua Bangi haiwez kuwa sakrament usichezee na mambo ya imani za watu
Like · Reply · 1 · 51 mins
Joe Ngutu Mkiambiwa bangi mbaya mnabisha, ona sasa ushuzi wako huu, tupe verse na tusome wapi kwenye kitabu chenu, maana wakristo wana biblia na waislamu wana Qur'an, je kitabu cha dini yenu kinaitwaje tukisome? Siyo umevuta tu mibangi yako ukadhani kila mtu ni mpuuzi mwezako, unaacha kujiita jina la baba yako mzazi unadandia jina la Nyerere kutafuta umaarufu ushuzi wakati kwenu ni Iringa mjinga sana wewe.
Like · Reply · 2 · 48 mins
Alex Ferguson huyo Yericko Nyerere anapaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kuhamasisha utumiaji wa madawa ya kulevya
Like · Reply · 1 · 45 mins
Vero Deo Jaman Yericko Nyerere hapo kufananisha bangi na sakrament cyo poa
Like · Reply · 1 · 41 mins
Nuswe Mwakinyuke Din ya wavutabang,waliochanganyikiwa akili,nasikitika kuona yeriko umekubwa na mkumbo
Like · Reply · 37 mins

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni