Jumatano, 20 Aprili 2016

Ugonjwa wa ajabu unao shambulia ngozi ya kinywa, pua na jicho wadaiwa kukosa tiba hospitali kubwa Mkoani Mbeya!

Na Emanuel Lengwa- Mbarali, Mbeya

Mtoto Stella Mdundwige.
Mama mzazi wa mtoto Stella
Kutoka upande wa kulia alie mshika bega mtoto Stella ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mkunywa Joshua Jackson Tenda na Kushoto ni mama mzazi wa mtoto Stella pamoja na wanafunzi wenzie.

 Mtoto Stella Mdundwige ambaye ni mwanafunzi wa wa darasa la nne katika katika shule ya msingi Mkunywa, Kata ya Madibira Wilayani Mbarali ameshindwa kuendelea na masomo baada ya kuugua ugonjwa wa ajabu unaoshambulia ngozi ya kinywa, macho na pua.

Mtoto Stella Mdundwige anadaiwa kua amekosa matibabu katika hospital zote kubwa mkoani Mbeya, hali ambayo imemfanya yeye na wazazi wake kuomba msaada wa matibabu katika hospital nyingine.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mkunywa, Joshua Jackson Tende amesema kuwa kutokana na kupatwa na ugonjwa huo mtoto Stella amelazimika kukatisha masomo, hivyo akaiomba serikali kuingilia kati ili kumrejesha mtoto huyo masomoni.

Baadhi ya wananchi na viongozi wa kata ya Madibira wamesema kuwa wao kama jamii wamejitahidi kusaidia kumfikisha mtoto huyo Hospitalini, lakini jitihada zo zimekwama kutokana na ugonjwa huo kukosa Tiba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni