1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki
yako.
2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa
mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.
3. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka
kituo gani, ni haki yako.
4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama
hukuambiwa sababu ya kukamatwa.
5. Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa
mhalifu ni haki yako kujikinga naye.
6. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika
suruali kama hujakataa kukri amri halali.
7. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa
mtuhumiwa halisi.
8. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha
kupekua.
9. Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.
10. Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la
mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.
11. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12
asubuhi.
12. Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili
asipandikize kitu.
13. Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.
14. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na
askari aweke sahihi.
15. Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.
16. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa
mwanaume.
17. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi
hazikufuatwa.
18. Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.
19. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo
chini ya ulinzi, ni haki yako.
20. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki
yako.
21. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea
shida.
22. Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya
ulinzi.
HIZI ZOTE NI HAKI ZAKO, USIZIOMBE
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni