Jumapili, 8 Mei 2016

Ajeruhiwa vibaya na wananchi baada ya kumbaka mama yake mzazi, dada yake na majirani wawili!

Kijana mmoja mjini Musoma anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumbaka mama yake mzazi, dada yake na wanawake wawili jirani wa familia hiyo.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’anzi alisema kwamba tukio hilo lilitokea  jumanne iliyopita majira ya saa 10 alasiri wakati mama wa kijana huyo alipofika nyumbani kutoka kazini akiwa na mtoto wake wa kike.

Akisimulia mkasa huo Ng’anzi alisema baada ya mama huyo kufika nyumbani na mtoto huyo kijana huyo alimvamia na kumbaka huku rafiki yake mbakaji huyo akilinda mlango wa kutokea ili kumzuia mama yake na dada zake wasiweze kukimbia.

Wakati kijana huyo akitekeleza unyama huo dhidi ya mama yake mzazi inaelezwa kua kulikua na vijana wengine ambao ni marafiki wa kijana huyo walikua wakilinda getini ili kuwazuia mama yake na dada yake  wasitoroke.

Kamanda alisema kua kijana huyo alipomaliza kumtendea ukatili mama na dada yake alimwamuru mama yake mzazi kuwapigia simu marafiki zake ili wafike nyumbani hapo haraka iwezekananvyo na walipofika kijana huyo aliwateka huku akiwatishia kwa panga na kuwabaka kwa kuwaingilia kinyume na maumbile.

Kijana huyo baada ya kumaliza kutenda ukatili huo aliwapiga picha wanawake hao wakiwa uchi kwa kutumia simu yake ya mkononi na kisha kuwaamuru kuondoka katika nyumba hiyo bila kelele, pia waliwatishia kwa kuwaambia kua wasithubutu kusema popote kuhusu ukatili aliowatendea na kwamba endapo wangetoa taarifa sehemu yeyote basi angewaua.

Baada ya akina mama hao kuruhusiwa kuondoka walienda kwa jirani zao na kutoa taarifa na baada ya taarifa hizo majirani walijikusanya na kwenda kuwavamia vijana hao wakiwa na silaha za jadi kwa ajili ya kujihami sambamba na kutoa taarifa kituo cha polisi ambapo polisi walifika eneo la tukio na kuwakuta wananchi wakiwa wamewakamaka vijana wawili sambamba na kuwajeruhi vibaya,

Baada ya polisi kuwasili katika eneo la tukio walilazimika kuwapeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa ajili ya matibabu wakiwa chini ya ulinzi wa polisi hivyo watafikishwa mahakamani muda wowote afya zao zitakapo imarika.

Baadhi ya majirani wakizungumzia tukio hilo walisema kua kijana huyo ni kibaka mzoezi na kwamba si mara yake ya kwanza kumbaka mama yake na tayari ameshawahi kufungwa jela na kwamba alikua hana muda mrefu uraiani toka atoke gerezani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni