Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi Nureyn, Sheikh Said Ahmed Abri akitoa hotuba yake kwa wageni waalikwa (Hawapo pichani) wakati wa hafla hiyo.
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imepongeza juhudi za Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Kiislam ya hapa nchini ya Dhi Nureyn Islamic Foundation kwa juhudi zake za kuunganisha nguvu na taasisi zingine za nje katika kuokoa maisha ya watoto wanaosumbuliwa na matatizo ya moyo.
Akizungumza wakati wa hafla maalum ya kufunga kambi ya Moyo Muhimbili, Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amebainisha kuwa, Serikali inatambua juhudi za taasisi binafsi katika kusaidiana nazo hivyo kwa hatua hiyo, suala la magonjwa ya moyo ambayo awali yalikuwa yakitibiwa nje kwa sasa yatashughulikiwa hapa hapa nchini.
“Tunaishukuru taasisi ya Dhi Nureyn na taasisi zote kwa kushirikiana na taasisi ya JKCI, kwani zimeweza kusaidia kuokoa maisha ya watanzania ikiwemo kuokoa vifo ambavyo vingetokea kwa watoto wenye matatizo ya moyo.
Zoezi hili limeweza kuvuka lengo la asilimia 70. Kwa wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa matibabu hayo ya moyo. Tunaamini mwaka huu tukaongeza malengo, na tayari wameweza kufanya operesheni takribani 200. Hii ni misheni ya pili na kwa maana hiyo wameweza kuvuka malengo ya asilimia 70 yale tuliyowapa.” Alieleza Dk. Kigwangalla.
Kigwangalla amesema, awali kabla ya utaratibu wa JKCI, wagonjwa 250 walikuwa wanapelekwa nje kufanyiwa operesheni hizo za magonjwa ya moyo. Lakini kwa mwaka huu hata miezi sita bado haijafika, Wagonjwa zaidi ya 200 wameshafanyiwa hapa hapa nchi operesheni hizo. Kwa hatua hiyo wameweza kuvuka lengo la asilimia 70 na wanataka wafikie angalau wagonjwa 400 hadi 500 kwa mwaka” alimalizia Dkr. Kigwangalla.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya Dhi Nureyn, Sheikh Said Ahmed Abri alieleza kuwa, taasisi hiyo imekuwa kiungo kuzitafuta taasisi zingine za nje ya nchi na kuleta wataalam hao bingwa wa magonjwa ya moyo hapa nchini.
Miongoni mwa taasisi hizo zilziofanikisha kambi hiyo ya Moyo hapa nchini ni pamoja na Taasisi ya Muntada Aid ya Uingereza, Timu ya Madaktai kutoka Saud Arabia, Taasisi ya RAF kutoka Qatar, Taasisi ya Dhi Nureyn (Tanzania) na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (Tanzania). Zoezi hilo la kambi ya magonjwa ya moyo ni la pili kufanyika hapa nchini likiwemo la kwanza la mwezi Mei mwaka jana (2015) na kufanikiwa kuwatibu watoto 66 wa Kitanzania ambao walipangiwa kwenda kutibiwa nje ya nchi na kufanya kuokoa mabilioni ya shilingi ya Serikali kwa ajili ya gharama za matibabu hayo.
“Tunaishukuru sana taasisi ya Muntada Aid, kwa kujali, kuthamini na kujitolea kufanya kazi hii iliyookoa maisha ya Watoto wengi na kuwaondoshea maumivu watoto na wazazi wao na kuwapa matumaini mapya ya maisha.
Sheikh Said Ahmed Abri katika hotuba yake ametoa shukrani kwa Taasisi ya Jakaya Kikwete na Wizara ya Afya na Serikali kwa ujumla pamoja na washirika wetu wote wakiwemo Taasisi ya Al Akhlaaq na wanahabari na wote kwa ujumla pamoja na mdaktari.
Aidha, madaktari hao pamoja na taasisi zote zilizofanikisha zoezi hilo, zilitunukiwa vyeti na tunzo maalum kwa ajili ya shukrani.
|
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akipiga picha ya pamoja na Madaktari bingwa wa Moyo . Mwenye kanzu nyeupe ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Sheikh Said Ahmed Abri, akifuatiwa na Daktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya Moyo, Profesa Joom Joom na mwingine ni daktari wa magonjwa ya Moyo aliyeambatana na timu hiyo ya madaktari hapa nchini
|
Daktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya Moyo, Profesa Joom Joom akielezea jambo kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani) namna walivyoweza kufanikisha Operesheni zilizofanyika hapa nchini hasa kwa watoto waliokuwa na matatizo ya Ugonjwa wa Moyo. Operesheni hiyo maalum ilifanyika kuazia Aprili mwaka huu na kumalizika mwezi huu wa Mei. Hafla hiyo imefanyika jana Mei 6.2016 Jijini Dar es Salaam. |
Baadhi ya Madaktari wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete wakifuatilia hafla hiyo |
Prof. Jameel Alata ambaye ni kiongozi wa Madaktari Mwelekezi wa Magonjwa ya Watoto akitoa shukrani zake kwa namna walivyoweza kufanikisha kambi hiyo ya Moyo hapa nchini. |
Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi Nureyn, Sheikh Said Ahmed Abri akimkabidhi tuzo Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi katika kuthamini taasisi hiyo. |
Baadhi ya Madaktari waliokabidhiw vyeti vya shukrani: |
Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi Nureyn, Sheikh Said Ahmed Abri akiabidhi tuzo kwa mgeni rasmi, Mh. Dk. Kigwangalla kwa namna Serikali inavyothamini mchango wa taasisi binafisi hapa nchini. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni