Jumamosi, 14 Mei 2016

Barozi wa Papa nchini Tanzania Askofu Mkuu Francisko Montecillo Padilla asema Siasa za kidunia zisiwe chanzo cha Utengano - Mbeya

Barozi wa Papa akitoa Baraka kwa maelefu ya waumimi na wakazi wa Mkoa wa Mbeya na Songwe waliofika kumlaki katika Uwanja wa Ndege wa Songwe, kulia kwake ni Askofu Evarist Chengulawa Jimbo Katoliki la Mbeya

Barozi wa Baba Mtakatifu,nchini Tanzania,Askofu Mkuu Francisko Montecillo Padilla  amewataka  waumini  wote wa imani mbalimbali kuishi kwa upendo,haki na  amani katika maisha yao ya kila siku  na kwamba  siasa za kidunia zisiwe chanzo cha utengamano bali ziwe sehemu ya upatanisho.

Akitoa mahubiri hapo jana katika ibada ya misa takatifu ya kipaimara  katika kanisa  la Mtakatifu Patrick,Parokia ya Vwawa,Jimbo Katoliki la Mbeya,Balozia,Padilla amesema Baba Mtakatifu Francisco  amekuwa akiwaalika  wanadamu kutafakari katika nyanja ya kisiasa kuhusu mshikamano  badala ya utengano.

Katika mazungumzo yake na waumini Padilla amesisiza upendo, haki na kuheshimu utu wa mtu binafsi na watu wengine ili kudumisha amani na kusisitiza kua binadamu wote ni sawa na viumbe wa mungu.

Mwakilishi huyo wa Papa  ameendelea kusisitiza kwa kutoa mfano wa kipofu aliyepata matumaini ya kuona na hatimaye mwenyezi mungu alimsaidia na kupata kuona vivyo hivyo kwa  wanadamu waishi kwa kuiga mfano huo.

Hata hivo Padilla alienda mbali zaidi na kusisitiza kuishi kwa ukarimu, upendo, kujitolea,kusamehe na kusaidia wengine wenye uhitaji kwani kwa kufanya hayo utaishi maisha yenye furaha ikiwa sambamba na kujipatia baraka tele kutoka kwa mwenyezi mungu.

Baadhi ya waumini na wakazi wa Vwawa waliojitokeza kumlaki Balozi huyo  sanjari na kusali naye, wamesema tukio la ujio wa barozi huyo nila kihistoria, Doria Namwazembe mkazi wa Vwawa akizungumza kwa furaha kubwa alisema kua anamshukuru mungu kwa ujio huo wa barozi huyo kwani ni baraka kubwa.

Kwa upande wao Francisca Mdoe  na Basilisa Sanga wamesema ujio wa kiongozi huo si furaha kwa wakatoliki pekee bali ni furaha kwa watanzania wote ujiohuo umeleta faraja na furaha kwakua ni nadra sana kutembelewa na barozi wa baba na kuahidi kuzitumia vema baraka atakazo ziacha na kuyaishi maagizo hayo  kwa vitendo katika jamii  wanazoishi.

Balozi  wa Papa amehitimisha ibada hiyo kwa kutoa sakramenti takatifu kwa  watoto  53 kutoka katika dekania tatu za Uwanda,Vwawa na Chunya  ambapo amesema hii ni  ziara yake ya mwisho kwani Baba Mtakatifu amempangia kwenda kuwahudumia  wananchi wengine katika nchi  za falme za kiarabu,kuwait,emirates na kwingineko katika nchi takribani saba.
Shamra shamra za mapozi ya Barozi wa Papa Francisko Montecillo Padilla katika uwanja wa Ndege Songwe

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni