Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli amesema badala ya kuwapa wafanyabiashara leseni ya kuagiza sukari
kutoka ng'ambo serikali yenyewe ndio itaagiza sukari hiyo moja kwa moja.
Rais Magufuli ametoa kauli
hiyo baada ya kubaini uwepo wa maelfu ya tani kadhaa ya sukari ambayo ilifichwa
katika mabohari katika mikoa ya Arusha na Kilombero iliyoagizwa kutoka nje na
ile iliyonunuliwa kutoka kwenye kampuni za kusaga sukari nchini Tanzania.
Aidha rais amewaahidi
watanzania kua katika siku zijazo sukari itapatikana kwa wingi hapa Tanzania na
kuongeza kua serikali imekwisha agiza sukari na kwamba serikali haitowapa
leseni ya kuagiza sukari wale wote waliowafilisi watanzania na badala yake
serikali itafanaya kazi hiyo yenyewe.
''Serikali imeagiza na itauza sukari hiyo kwa bei ya chini,,,,
hilo ndio lengo la serikali '' alisema rais Magufuli huku mawananchi
wakimshangilia.
Hata hivyo serikali katika kuonesha kua ipo imara na haipo
tayari kuyumbishwa na baadhi ya wafanyabiashara wasio na nia njema na
watanzania imeanza kugawa sukari iliyoingizwa nchini kinyume cha sheria na
kufichwa katika mabohari kote nchini.
TRA ilichukua hatua hiyo
baada ya mwekezaji wa kibinafsi mkoani Lindi kupatikana na zaidi ya mifuko elfu
tano za sukari kutoka nga'mbo.
Yamkini sukari hiyo
hubadilishwa kwenye mifuko yenye nembo ya kampuni za kusaga sukari za Tanzania
na kisha kuuzwa kwa bei maradufu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni