Wakati nchini Tanzania baadhi ya viongozi wakinyoosheana vidole kwa madai kuwa baadhi ya viongozi hususani wanawake hupewa madaraka kwa kigezo cha kujihushisha kimapenzi na viongozi wa juu wa vyama vya siasa jambo ambalo linatafsiriwa kua wanawake hao hawana uwezo bali wanabebwa kwa nguvu ya mapenzi.
Shirikisho la Soka la Kimataifa jana limemteua Fatma Samba Diouf Samoura wa Senegal kuwa Katibu Mkuu wake (SG).
Shirikisho la Soka la Kimataifa jana limemteua Fatma Samba Diouf Samoura wa Senegal kuwa Katibu Mkuu wake (SG).
Mwanamama huyo mwenye uzoefu wa miaka 21 wa kufanya kazi katika Shirika la Umoja wa Mataifa, ambaye kwa sasa ni Mratibu Mkazi wa UNDP mchini Nigeria, uteuzi wake umetangazwa na Rais wa FIFA, Mtaliano Gianni Infantino katika Mkutano Mkuu wa 66 wa FIFA mjini Mexico City.
Rais wa FIFA alimwagia sifa mwanamama huyo kwa kusema “Fatma ni mwanamke mwenye uzoefu wa kimataifa ambaye ameshughulikia masuala mazito,” alisema Rais Infantino.
“Amethibitisha uwezo wa kutengeneza na kuongoza timu, na kuboresha namna utendaji wa oganazesheni. Muhimu kwa FIFA, anafahamu uwazi na ushirikishaji ni moyo wa mwenendo wowote mzuri,”.
Mama Samoura anatarajiwa kuanza rasmi kazi ya Ukatibu Mkuu katikati ya Juni.
Tangu ameanza kufanya kazi UN kama Ofisa mkubwa wa mradi chakula mjini Rome mwaka 1995, Mama Samoura amekuwa mwakilishi au Mkurugenzi wa mataifa sita; Djibouti, Cameroon, Chad, Guinea, Madagascar and Nigeria.
Kila la kheri Bi. Fatma Samba Diouf Samoura katika kutekeleza majukumu yako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni