Jumamosi, 14 Mei 2016

Mkazi wa Dodoma ahukumiwa kifungo ya miaka 30 jela kwa kuishi chumba kimoja na mtoto wake wa kumzaa kama mke na mume.


Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Dodoma, jana ilimhukumu kifungo cha miaka 30 jela, Bw. Godfrey Mjelwa mwenye umri wa miaka 48, baada ya kupatikana na hatia ya kuishi  kma mke na mume na binti yake wa kumzaa .

Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo, Mwajuma Lukindo alisema ushahidi wa pande zote ulithibitisha kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo la kuishi chumba kimoja na binti yake.

Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo , Mjelwa ambae ni mkazi wa mtaa wa Kizota katika Manispaa ya Dodoma,  alipatikana na hatia ya kuishi na  binti yake mwenye umri wa miaka 15 (jina limehifadhiwa). 

Aidha hakimu Lukindo alifafanua kua kosa alilokutwa nalo mtuhumiwa ni kufanya mapenzi na ndugu wa dam , licha ya kuwa mtoto huyo bado ni mdogo, lakini ni mtoto wake wa kumzaa.

Nae Mwendesha mashtaka Janeth Mgome, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa, ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia hiyo. 

Kwa upande wake mtuhumiwa alipotakiwa kujitetea alijikuta akiwaacha hoi baadhi ya mashuhuda waliokuwepo mahakamani hapo baada ya kuomba kupunguziwa adhabu kwa madai kuwa mtoto wake huyo bado mdogo kwa kuwa ana miaka 14 na miezi tisa na siku tisa, siyo miaka 15 kama ilivyodaiwa mahakamani hapo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni