Mchungaji wa kanisa la Moraviani Mkoani katavi wilaya ya Mlele
katika kijiji cha Usevya Bw. Godwel Godwel Siame amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Mkoa wa katavi kwa kosa la Uhujumu uchumi la kukutwa na meno ya
tembo yenye uzito upatao kilogramu 20 yenye jumla ya Thamani ya Tshs 90 m.
Akisoma hati ya Mashtaka mbele ya Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa
Mahakama ya Mkoa wa Katavi Mhe Chiganga Tengwa, wakili wa Serikali Jamila
Mziray ameileza Mahakama kwamba Mnamo tarehe 5 mwezi 2016 Mshitakiwa Mch.
Godwel alikutwa na nyara hizo zenye jumla ya Thamani ya 90 milioni zikiwa na
jumla ya Uzito wa kilogramu 20.
Mahakama ilimweleza Mshitakiwa kwamba hakutakiwa kujibu lolote juu
ya shitaka linalomkabili kwa kuwa mahakama hiyo haikuwa na mamlalaka ya
kuendelea (Pecuniary Jurisdiction) kufuatia thamani ya nyara hizo kuwa zaidi ya
Milioni 10.
Wakili aliendelea kuileza Mahakama kwamba upelelezi wa shauri hilo
haujakamilika na hivyo kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.
Mshitakiwa aliwakilishwa na wakili Msomi Patrick Amulike Mwakyusa ambae
ameiomba Mahakama kuitaka Jamhuri kuleta kibali cha kuruhusu na kuipatia
mamlaka Mahakama (certificate & consent) ya kuendelea na shauri hilo ili
Mshitakiwa apate haki yake ya dhamana kwa kuwa kosa hilo lina dhamana.
Kesi hiyo iliyosajiliwa kwa Na EC 41/2016 imeahirishwa na
kupangiwa tarehe nyingine ya kutajwa ambayo ni tarehe 23/5/2016.
Mshitakiwa amepelekwa Mahabusu mpaka tarehe iliyoamuriwa na
Mahakama atakapo rudishwa tena kizimbani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni