Ijumaa, 20 Mei 2016

Msanii Ali Kiba sasa kung'ara kimataifa baada ya kusaini mkataba mnono!




Staa wa Bongo Fleva, Ali kiba amesaini mkataba na kampuni ya Sony Music iliyopo jijini Johannesburg,South Africa, moja ya vitu vilivyomo kwenye mkataba huu ni kampuni hii kubwa ya muziki duniani kusimamia pia video zake na audio kwa kuzilipia na kuzifikisha kwenye masoko makubwa ya muziki duniani.

Ali Kiba ameungana na mastaa wengine duniani waliosign Sony Music kama Davido (Nigeria) , Chris Brown ( Marekani) ,John Legend na wengineo.

Baada ya kusaini mkataba na SonyMUSIC, miongoni mwa kazi zitakazo fanywa na kampuni hiyo ni kusimamia kazi zake za kimuziki duniani kote kwa kiwango cha kimataifa 

Ni msanii ambaye mara nyingi amekua aishindanishwa na Diamond Platnumz pia licha ya kuonekana kua ameshindwa kujitangaza kimataifa alakini amejitahidi sana kuweza kutoshuka katika muziki toka atoke ya kujulikana kama msanii mkubwa hapa nchini.

Pia amefanikiwa kuwahamasisha vijana wengi sana kuingia katika muziki na kuona nao wanaweza kutoka kwa njia ya muziki hata hivo ali kiba amekua akiwapa sapoti ya nguvu kwa kukubali kushirikishwa katika nyimbo  za  wasanii wadogo (underground),


Alikiba ameshirika katika nyimbo moja na R kelly katika project yake ya One8 ambayo ilichukuwa tuzo ya BET kama most inspirational song pia kiba mwaka 2014 alifanikiwa kuchukuwa tuzo tano za kili muziki awards na ngoma yake ya Mwana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni