JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA
WATOTO
TAARIFA KWA UMMA
Baraza la Tiba Asili na Tiba
Mbadala, Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto,
linawatangazia waganga wote wa tiba asili na tiba mbadala wanaotoa matangazo
kwenye vyombo vya habari bila kibali cha Baraza na wale wanaobadilisha kwa
kutangaza kinyume na maagizo ya Baraza baada ya kupewa kibali waache mara moja.
Hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaokiuka agizo hili kuanzia siku
saba (7) baada ya kutoka kwa taarifa hii.
Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala
linaendelea kusisitiza watoa huduma wote wa tiba asili na tiba mbadala
kujisajili, kusajili wasaidizi wao,vituo na maduka yao kabla ya mwezi wa sita.
Fomu za maombi ya usajili zinapatikana kwa Waratibu wa tiba asili na tiba
mbadala walipo katika ofisi za Waganga
Wakuu wa Wilaya (DMO). Waganga wote wanaotoa huduma bila kujisajili wanafanya
kosa kisheria na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Zingatia:
Vibali vyote vya usajili na matangazo vinatolewa na Baraza la Tiba Asili na
Tiba Mbadala chini ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto. Vibali na usajili wa serikali hautolewi na vyama vya waganga, shirika,
afisa utamaduni, polisi au mtu mwingine yeyote.
Imetolewa na
Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala
20/5/2016
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni